NI MATESO. Usisikie, wikiendi iliyopita ilikuwa ngumu sana kwa mashabiki wa Manchester United baada ya kushuhudia timu yao ikipigwa kama ngoma kwa kufumuliwa mabao 6-3 katika mechi ya Manchester Derby iliyopigwa kwenye Uwanja wa Etihad.
Katika mchezo huo ulioanza saa 10:00 jioni Man City ilijipatia mabao yake kupitia Erling Haaland na Phil Foden ambao kila mmoja alipiga hat-trick.