Prime
Wababe Simba walioichapa Yanga mara ya mwisho!
SIMBA imekubali vipigo sita mfululizo kutoka kwa Yanga, hali inayochangia Dabi ya Kariakoo kesho, Jumapili kusubiriwa nini kitatokea. Wekundu wa Msimbazi wataendelea kuonewa au watakataa unyonge na kufungua ukurasa mpya.
Rekodi zinaonyesha, mara ya mwisho Yanga kupoteza mechi mbele ya Simba ilikuwa Agosti 13, 2023 katika mechi ya Ngao ya Jamii iliyochezwa Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.
Katika mechi hiyo, dakika 90 matokeo yalikuwa 0-0, penalti zikaamua ushindi kwa Simba ikiichapa Yanga 3-1, huku kipa Ally Salim akiibuka shujaa kwa kupangua mikwaju mitatu ya Khalid Aucho, Pacome Zouzoua na Yao Kouassi.
Baada ya mechi hiyo, Yanga imetembeza vipigo sita mfululizo kwa Simba, vinne katika Ligi na viwili Ngao ya Jamii.
Ubabe wa Yanga kwa Simba katika Ligi Kuu Bara matokeo yalikuwa hivi; Simba 1-5 Yanga (Novemba 5, 2023), Yanga 2-1 Simba (Aprili 20, 2024), Simba 0-1 Yanga (Oktoba 19, 2024) na Yanga 2-0 Simba (Juni 25, 2025). Pia mechi mbili za Ngao ya Jamii matokeo yali kuwa hivi; Yanga 1-0 Simba na Yanga 1-0 Simba.
Ukiangalia vikosi vilivyoanza katika mechi ile ya mwisho ambayo Simba inapata ushindi mbele ya Yanga na kulinganisha hivi sasa, kuna mabadiliko makubwa.
Kwa kukukumbusha tu, kikosi cha Yanga kilichoanza kilikuwa na; Djigui Diarra, Yao Kouassi, Joyce Lomalisa, Bakari Mwamnyeto, Ibrahim Bacca, Khalid Aucho, Maxi Nzengeli, Mudathiri Yahya, Clement Mzize, Kennedy Musonda na Jesus Moloko.
Benchi alikuwepo Metacha Mnata, Nickson Kibabage, Dickson Job, Gift Fred, Jonas Mkude, Salum Abubakar 'Sure Boy', Pacome Zouzoua, Aziz Ki na Hafiz Konkoni.
Kwa upande wa Simba, walioanza ni Ally Salim, Shomari Kapombe, Mohamed Hussein, Kennedy Juma, Che Malone Fondoh, Sadio Kanoute, Clatous Chama, Mzamiru Yassin, John Bocco, Saido Ntibazonkiza na Luis Miquissone.
Waliokuwa benchi ni Hussein Abel, Israel Mwenda, Hussein Kazi, Fabrice Ngoma, Aubin Kramo, Willy Onana, Moses Phiri, Kibu Denis na Jean Baleke.
Jina: Ally Salim
Nafasi: Golikipa
Uraia: Tanzania
Alipo sasa: Dodoma Jiji
Jina: Shomari Kapombe
Nafasi: Beki wa kulia
Uraia: Tanzania
Alipo sasa: Bado yupo Simba
Jina: Mohamed Hussein
Nafasi: Beki wa kushoto
Uraia: Tanzania
Alipo sasa: Yanga SC
Jina: Kennedy Juma
Nafasi: Beki wa kati
Uraia: Tanzania
Alipo sasa: Singida Black Stars
Jina: Che Malone Fondoh
Nafasi: Beki wa kati
Uraia: Cameroon
Alipo sasa: USM Alger (Algeria)
Jina: Sadio Kanoute
Nafasi: Kiungo mkabaji
Uraia: Mali
Alipo sasa: Azam
Jina: Clatous Chama
Nafasi: Kiungo mshambuliaji
Uraia: Zambia
Alipo sasa: Amerudi Simba (aliondoka kwenda Yanga, kisha Singida BS)
Jina: Mzamiru Yassin
Nafasi: Kiungo wa kati
Uraia: Tanzania
Alipo sasa: TRA United (mkopo)
Jina: John Bocco
Nafasi: Mshambuliaji
Uraia: Tanzania
Alipo sasa: Kocha wa vijana Simba
Jina: Saido Ntibazonkiza
Nafasi: Kiungo mshambuliaji
Uraia: Burundi
Alipo sasa: Vital'O FC (Burundi)
Jina: Luis Miquissone
Nafasi: Kiungo mshambuliaji
Uraia: Msumbiji
Alipo sasa: Al-Ahly SC (Libya)
Jina: Hussein Abel
Nafasi: Golikipa
Uraia: Tanzania
Alipo sasa: Bado yupo Simba
Jina: Israel Mwenda
Nafasi: Beki wa kulia
Uraia: Tanzania
Alipo sasa: Yanga SC
Jina: Hussein Kazi
Nafasi: Beki wa kati
Uraia: Tanzania
Alipo sasa: Namungo
Jina: Fabrice Ngoma
Nafasi: Kiungo mkabaji
Uraia: DR Congo
Alipo sasa: Al-Nasr SC (Libya)
Jina: Aubin Kramo
Nafasi: Winga
Uraia: Ivory Coast
Alipo sasa: Ittihad Gharyan SC (Libya)
Jina: Willy Onana
Nafasi: Mshambuliaji
Uraia: Cameroon
Alipo sasa: CS Sfaxien (Tunisia)
Jina: Moses Phiri
Nafasi: Mshambuliaji
Uraia: Zambia
Alipo sasa: Green Eagles FC (Zambia)
Jina: Kibu Denis
Nafasi: Mshambuliaji
Uraia: Tanzania
Alipo sasa: Al-Nasr SC (Libya)
Jina: Jean Baleke
Nafasi: Mshambuliaji
Uraia: DR Congo
Alipo sasa: Al-Khums SC (Libya)
KOCHA: Roberto Oliveira 'Robertinho'
Uraia: Brazil
Alipo sasa: Jeddah SC (Saudi Arabia)