Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Utamu wa dabi upo hapa!

PRESHA Pict


Dabi ya Kariakoo, Yanga dhidi ya Simba, siyo  mchezo wa kawaida wa ligi. Ni pambano la heshima, historia na presha ya mashabiki. Lakini zaidi ya mbinu za makocha na majina ya wachezaji, mara nyingi huamuliwa na vita binafsi uwanjani, nani anamshinda nani katika eneo lake.


Keshokutwa, Jumapili 'Machi Mosi' macho yote yatakuwa kwenye Uwanja wa New Amaan Complex, visiwani Zanzibar kwenye mapambano ya moja kwa moja kuanzia safu ya ushambuliaji, kiungo hadi ulinzi na langoni.

PRESH 06

De Reuck vs Dube

Hapa kuna bato ya maana katika safu ya ulinzi ya Simba, beki wa kati Rushine De Reuck atakuwa na  kazi ya kumkaba mshambuliaji Prince Dube wa Yanga. Hii ni vita ya kimwili na kiakili.

Dube ni mshambuliaji anayependa kucheza kwa kutumia mwili wake. Mara nyingi hupokea mpira akiwa ameligeuzia lango mgongo, kisha hutumia nguvu na ustadi kujigeuza au kutoa pasi ya haraka kwa mchezaji anayeingia kwa kasi. Hii inamaanisha De Reuck atalazimika kuwa karibu naye, kumzuia asipate muda wa kujiweka sawa.

PRESH 07

Iwapo Dube ataachwa huru, ana uwezo wa kupiga shuti kali au kulazimisha faulo karibu na boksi. De Reuck atalazimika kushinda vita ya kusimama imara (body positioning, hii ni mechi ambayo makosa madogo ya kiulinzi yanaweza kuzaa bao.

PRESH 05

Toure vs Depu

Kuna vita nyingine hapa kati ya beki mwingine wa Simba, Ismail Toure dhidi ya Laurindo Dilson ‘Depu’ . Tofauti na Dube, Depu ni mshambuliaji mwenye kasi anayependa kukimbia nyuma ya mabeki.

Wote wawili ni mara yao ya kwanza kucheza dabi ya Kariakoo, Depu alitokea Radomiak Radom ya Ureno lakini kwa upande wa Toure alijiunga na Simba dirisha dogo akitokea FC Baniyas ya Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) .

Depu hutegemea  mipira ya kupenyeza na kukimbia kwenye nafasi zilizoachwa wazi. Hivyo Toure atalazimika kuwa makini na mstari wa ulinzi. Hatua moja ya kuchelewa au kukosa mawasiliano na beki mwenzake inaweza kumwacha Depu ana kwa ana na kipa.

PRESH 08

Mbali na hilo mshambuliaji huyo mwenye mabao matano Ligi Kuu na mawili ya Ligi ya Mabingwa Afrika ni mzuri kwenye mipira ya vichwa hasa wakati Yanga inapata kona au zinapopigwa krosi za mabeki wa pembeni.

Kwenye mabao hayo saba matatu amefunga kwa kichwa jambo ambalo  Toure  atahitaji kutumia nguvu yake kuzuia kasi, pia akili ya kusoma pasi mapema kama atamruhusu Depu apate nafasi ya kwanza, Simba wanaweza kuadhibiwa haraka.

PRESH 02

Job vs Mwalimu

Kwa upande wa Yanga, mabeki Dickson Job, Ibrahim Hamad ‘Bacca’ na Bakari Mwamnyeto kati ya hao kila mmoja ana nafasi ya kuanza kikosini kutokana na umuhimu wao kwenye eneo la ulinzi.

Msimu huu hadi sasa eneo la mabeki wameruhusu mabao mawili pekee sawa na safu ya ulinzi ya Azam iliyoruhusu idadi hiyo zikiwa timu pekee zilizotikiswa nyavu zao mara chache.

Mbele yao kuna washambuliaji wawili wa Simba, Selemani Mwalimu mwenye mabao matatu na Baraka Mwangosi  ambao wanaongoza safu ya ushambuliaji ya timu hiyo.

PRESH 04

Mwalimu ni mshambuliaji anayependa kucheza ndani ya boksi, hasa kwenye mipira ya krosi. Hii ina maana mabeki hao watalazimika kushinda mipira ya juu na kumzuia asiruke. Mwamnyeto kwa uzoefu wake wa dabi amekuwa mzuri wa kuishinda mipira ya juu.

Kama Simba wataamua kutumia zaidi mashambulizi ya pembeni, basi vita hii itakuwa ya kimwili kwa dakika zote 90. Lakini kama Job, Bacca  na Mwamnyeto watawafanya washambuliaji hao wacheze nje ya boksi, wataipunguza makali ya Simba.


VITA YA VIUNGO

Hapa ndipo ilipo dabi yenyewe sasa , kiungo mkabaji wa Simba, Yusuph Kagoma ni mmoja ya viungo wanaosifika kwa kukaba na pasi zake kufika kwa mlengwa  atakuwa na jukumu la moja kwa moja la kumzuia Mudathir Yahya wa Yanga.

Mudathir ni kiungo anayependa kupokea mpira katikati ya mistari ya ulinzi na kiungo. Akipewa nafasi ya kugeuka, anaweza kupiga pasi ya mwisho au kupiga shuti la kushtukiza. Kagoma atalazimika kumkaba mapema kabla hajageuka kupenyeza pasi.

Hii ni vita ya akili. Mudathir anaweza kujaribu kumvuta Kagoma nje ya eneo lake ili kufungua nafasi kwa wenzake. Lakini Kagoma akifanikiwa kumzuia asipokee mpira kwa uhuru, Yanga wanaweza kupoteza ubunifu wao katikati.

PRESH 03

Camara vs Abuya

Naby Camara wa Simba na Duke Abuya wa Yanga kuna vita nyingine ya kudhibiti kasi ya mchezo.Camara ni kiungo wa nguvu anayependa kukimbia na mpira na kuongeza kasi ya mashambulizi. Abuya ni mtulivu zaidi, hupendelea pasi za uhakika na kudhibiti mechi.

PRESH 01

Iwapo Camara atavunja mpangilio wa Yanga kwa mbio zake na pasi ndefu, Simba watakuwa na presha kubwa mbele. Lakini kama Abuya atadhibiti mipira na kuilazimisha Simba kukimbia bila mpira, Yanga watafaidika kwa umiliki na utulivu.


Vita ya Makipa

Langoni kwa Yanga, Djigui Diarra ana uzoefu mkubwa wa mechi zenye presha ya dabi si mara yake ya kwanza amekuwa na mawasiliano mazuri na mabeki wake na ana uwezo wa kuokoa mipira ya hatari katika wakati mgumu.

Ingawa ni mzoefu lakini golikipa huyo namba moja wa timu ya taifa ya Mali amekuwa na makosa hasa kwenye mipira ya kona ambayo Simba imekuwa ikiitumia vizuri hasa kwa beki wa kati, De Reuck mwenye mabao matatu.

Kwa Simba, Djibrilla Kassali ni mara yake ya kwanza kucheza dabi na  alisajiliwa dirisha dogo akitokea AS Fan ya Niger. Simba ilimnunua dakika za mwishoni baada ya makipa wake tegemeo kuumia, Mousa Camara na Yakoub Suleimani kuumia.

Tayari amecheza mechi tatu za Ligi Kuu dhidi ya Mashujaa, Dodoma Jiji na Tanzania Prisons n azote ameondoka na cleansheet, ana uwezo wa kuokoa mipira ya karibu ana utulivu lakini amekuwa na udhaifu kwenye mipira ya mbali.

Iwapo Dube au Depu watapita kwenye eneo ulinzi wa Simba, Kassali atalazimika kufanya maamuzi ya haraka. Vivyo hivyo, kama De Reuck au Mwalimu atapata nafasi ya kichwa ndani ya boksi, Diarra atahitajika kuwa makini.