Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ubora wa Manula Simba unavyotesa makipa

MANULA Pict


DJIBRILLA Kassali ndio jina la kipa mpya ndani ya kikosi cha Simba ambaye amesajiliwa katika dirisha hili la usajili lililofungwa Januari 31 mwaka huu.


Usajili wa kipa huyo umefanyika mapema baada ya kuumia kwa makipa wa timu hiyo akiwmo, aliyekuwa kipa namba moja Mousa Camara ambaye tayari ameondolewa kwenye mfumo baada ya usajili huo mpya.


Hiyo ni kwa mujibu wa kanuni ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), ambayo inazitaka timu zinazoshiriki Ligi Kuu Bara kufanya usajili wa kipa mmoja wa kigeni. Kuumia kwa Yacoub Suleiman, kipa namba mbili wa timu hiyo ambaye ni mzawa, kulichangia kusajiliwa kwa Kassali.

Yacoub alipata majeraha kwenye goti lake katika mazoezi ya mwisho ya kujiandaa na mchezo wao wa ufunguzi wa fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON) 2025 dhidi ya Nigeria, majeraha yaliyotarajiwa kumuweka nje ya uwanja kwa muda mrefu na alikosa michuano yote ya AFCON iliyomalizika nchini Morocco.

MANU 01

Taarifa hiyo ilitolewa na madaktari wa timu hiyo kutokea nchini Morocco na hadi sasa kipa huyo sio sehemu ya kikosi cha Simba anaendelea na kujitibia akiwa nje ya kikosi ambacho sasa kinasimama na kipa mpya Kassali na mzawa Hussein Abel.

Hali inayopitia sasa timu hiyo ya kusajili makipa kila msimu ni wazi kwamba wekundu hao wanaandamwa na ‘mzimu’ wa Aishi Manula, kipa aliyedumu muda mrefu kikosini hapo na kuondoka na rekodi kibao za kibabe akiliweka jina lake miongoni mwa makipa bora nchini na Afrika.

Swali ni je, Kassali ataweza kufikia rekodi ya Manula ndani ya Simba kucheza misimu zaidi ya miwili au hata kumaliza mkataba wake wa miaka miwili aliosaini na timu hiyo ili kukwepa changamoto inayowakumba makipa kwa miaka ya hivi karibuni?

Ipo hivi. Kwa miaka ya hivi karibuni Simba imesajili makipa zaidi ya watano tangu Manula achukue ufalme ndani ya kikosi hicho Msimbazi alichojiunga nacho akitokea Azam FC Agosti 2017.

MANU 02

Manula ndiye kipa pekee aliyehudumu muda mrefu ndani ya timu hiyo katika miaka ya hivi karibuni akiipa mafanikio katika michuano ya ndani na kimataifa, lakini wengine wote baada ya hapo hawajawa na misimu mingi licha ya kwamba aliondoka Simba msimu uliopita baada ya kumaliza mkataba wake.

Kabla ya Manula kusepa Simba, uongozi ulifanikiwa kunasa saini ya Ayoub Lakred aliyetua 2023/24 kwa mkataba wa mwaka mmoja akitokea FAR Rabat ya Morocco baada ya kuipa ubingwa wa Ligi Kuu timu hiyo.

Usajili wa Ayoub ulikuwa wa ghafla Simba kwani tayari ilikuwa imesajili kipa Mbrazili Jefferson Luiz ambaye aliishia Misri kwenye kambi ya maandalizi ya msimu (pre season) baada ya kupata majeraha.

Na Lakred licha ya kutoka kutwaa taji Morocco hakuanza msimu vizuri na alianza kupata nafasi baada ya Manula kuumia, huku ule msimu wa kwanza Ayoub akicheza mechi 14 za ligi kwa dakika 1,260 na kuondoka na ‘clean sheets’ nane akiruhusu mabao 10. Lakred aliongeza mkataba uliomalizika msimu uliopita.

MANU 03

Itakumbukwa kwamba Lakred aliondoka Simba akiwa ameichezea kwa msimu mmoja mzima, lakini uliofuata hakuuanza wala kuumaliza akiwa golini kwani aliumia akiwa kambini Uturuki, ambako timu hiyo ilikuwa katika maandalizi ya msimu, suala ambalo liliulazimu uongozi wa Wekundu wa Msimbazi kumsajili Camara, ambaye kwa sasa ni majeruhi akiwa ndani ya msimu wake wa pili.


MANULA SASA

Manula aliumia Machi 22, 2024 akiwa anaitumikia timu ya taifa ya Tanzania (Taifa Stars) katika michuano maalumu ya Fifa Series iliyofanyika Baku, Azerbaijan.

Lakini, hata kabla ya michuano hiyo kipa huyo alikuwa ameingia kwenye sintofahamu na Simba, kwani katika mechi nyingi za mashindano ama hakuwepo kabisa benchini au alisugua huku Camara akicheza. Ikumbukwe kwamba wakati Manula akisugua pia Lakred alikuwa hajamaliza mkataba Msimbazi, ambapo golini asipodaka Camara alisimama Ally Salim kama msaidizi wake.

Katika mchezo dhidi ya Bulgaria uliochezwa Dalga Arena ambako timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars ilipoteza kwa bao 1-0, Manula alitoka uwanjani katika dakika ya 31 na nafasi yake ikachukuliwa na Kwesi Kawawa.


LAKRED NAYE

Lakred alikuwa miongoni mwa makipa waliotegemewa na Simba, lakini baada ya kucheza msimu mmoja na uongozi kumuongezea mkataba wa miaka miwili, matumaini hayo yalikatizwa baada ya kupata jeraha kubwa wakati wa maandalizi ya msimu 2024/25 nchini Misri.

Katika kipindi hicho, Simba ilikuwa kwenye harakati za kujiandaa kwa mashindano makubwa, jambo ambalo lilisababisha usajili wa Camara. Ujio wa Camara ndani ya Simba uliwasahaulisha mashabiki uwepo wa Lakred kutokana na ubora alioanza nao kipa huyo ambaye pia amecheza msimu mmoja uliopita akimaliza kinara Ligi Kuu Bara akiwa na ‘clean sheets’ 19 ukiwa ni msimu wake wa kwanza kati ya miwili Msimbazi.

Licha ya kuanza vizuri msimu akiwa na timu hiyo, Camara ambaye alijimilikisha namba akimuondoa kabisa Manula, ambaye mkataba wake ulipomalizika akatua Azam FC, naye pia akaumia kwa muda mrefu hadi kuwalazimu mabosi kurudi sokoni na umlea Kassali katika usajili wa dirisha dogo. Iwapo Camara ataondoka Simba ataacha swali moja; kuna nini? Kwani hakuna kipa baada ya zama za Manula atakayekuwa amedumu muda mrefu katika milingoti Msimbazi.

MANU 04

MOUSSA CAMARA

Alijiunga na Simba msimu uliopita kwa mkataba wa miaka miwili msimu wake wa kwanza ndani ya kikosi hicho alitoa picha kwamba ndiye mbadala sahihi wa Manula kwani alifanya vizuri kwa kuibuka kipa bora wa msimu akimuacha kipa namba moja wa Yanga, Djigui Diarra.

Camara aliibuka kipa bora wa Ligi Kuu Bara kwa msimu wa 2024-2025, baada ya kumaliza na 'Clean Sheets' 19, ikiwa ni msimu wake wa kwanza nchini tangu ajiunge na kikosi hicho akitokea Horoya AC ya kwao Guinea.

Kipa huyo aliibuka kipa bora baada ya mshindani wake mkubwa, Diarra wa Yanga kukosekana katika mechi dhidi ya Dodoma Jiji iliyopigwa kwenye Uwanja wa New Amaan Complex visiwani Zanzibar, ambayo alicheza nyota mwenzake, Aboutwalib Mshery na kuweka clean sheet

Diarra alikosa tuzo hiyo kwa msimu wa pili mfululizo baada ya msimu uliotangulia wa 2023-2024, kumaliza na 'clean sheets' 14, akizidiwa ujanja na aliyekuwa kipa wa Coastal Union, Mkongomani Ley Matampi aliyeshinda tuzo ya Kipa Bora wa Msimu kwa 'clean sheets' 15.

Camara ambaye ameondolewa kwenye mfumo wa usajili Simba, msimu wake wa kwanza alicheza mechi 28 alitumika kwa dakika 2520 aliruhusu nyavu zake kutikiswa mara 13 na kupata 'clean sheets' 19 zilizompa tuzo.

Msimu huu ambao ndio ulikuwa wa mwisho kwake ndani ya klabu ya Simba baada ya kusaini mkataba wa miaka miwili amecheza mechi moja kwa dakika zote 90 hadi hapo alipobainika kuwa ana shida ya goti ambalo walienda kulifanyia upasuaji na kumuweka nje ya uwanja hadi sasa ambapo ameondolewa kabisa kwenye mfumo wa usajili.

MANU 06

YAKOUB SULEIMAN

Mara baada ya Camara kuumia akiwa nje ya uwanja kwa muda uongozi wa Simba ulimuamini kipa huyo ambaye alijiunga na Simba mwanzoni mwa msimu uliopita akitokea JKT Tanzania.

Yakoub Suleiman hakukaa kinyonge mara baada ya kupata nafasi hiyo ambapo msimu huu amecheza mechi nne za Ligi Kuu ambapo ametumika kwa dakika 360 na kwenye dakika hizo ni mechi moja pekee ndio hajaruhusu nyavu zake kutikiswa, akiruhusu mabao matatu.

Baada ya kuaminiwa na kupewa nafasi, alionyesha uwezo mkubwa ambao ulimshawishi kocha wa timu ya taifa kumuita Taifa Stars ambako ndiko alikopata majanga yaliyomuweka nje ya uwanja hadi sasa na kusababisha Simba kumleta kipa mpya, Kassali.

  • MANU 05

REKODI MANULA MATAJI (11)

Katika kipindi cha miaka mitano, Manula aliiwezesha Simba kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara mara nne mfululizo (2017/18), (2018/19), (2019/20) na 2020/21.

Mbali na ligi alichukua pia mataji mawili mfululizo ya Kombe la Shirikisho la Azam maarufu (ASFC) msimu wa 2019/2020 na 2020/2021.

Ngao ya Jamii aliibeba mara nne mfululizo tangu 2017-2020 akiwa na kikosi hicho ambacho ndicho kinaongoza kutwaa taji hilo mara tisa (9) tangu lilipoanzishwa rasmi 2001, kombe jingine likiwa ni la Mapinduzi alilotwaa mwaka 2022.


TUZO BINAFSI

Manula (26) ndiye anayeongoza kwa rekodi ya kuchukua tuzo nyingi (5) za Kipa Bora wa Ligi Kuu Bara kwenye nafasi anayocheza kwa kizazi cha sasa.

Manula alitwaa tuzo hizo misimu ya 2015/2016, 2016/2017 akiwa na Azam FC, huku akiwa na Simba ni 2017/2018, 2019/2020, 2020/21 kisha msimu wa 2021/22 alipinduliwa na Djigui Diarra wa Yanga ambaye nyavu zake hazikuguswa mara 15.

Endapo msimu wa 2018/19 ungekuwa na tuzo basi Manula angekuwa anamiliki sita, kwani aliiwezesha timu yake kunyakua ubingwa kwa kufikisha pointi 93 huku akifungwa mara 15.


HANA MPINZANI

Tangu kuwasili kwenye kikosi hicho, Manula amekutana na makipa wengi ila hadi sasa hakuna aliyeleta ushindani kwake wa kutishia nafasi yake hali inayomfanya kuendelea kutamba kila uchao. Miongoni mwa makipa hao ni Emmanuel Mseja, Said Mohamed ‘Nduda’, Deogratius Munish ‘Dida’, Jeremiah Kisubi, Ally Salim na Beno Kakolanya.