Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

SOKONI KUBAYA: Mbappe, Osimhen hawachekani ishu ya thamani zao kushuka maradufu

SOKONI Pict

Muktasari:

  • Thamani ya mchezaji kupanda sokoni ni kitu kinachofurahiwa na karibu kila mtu, lakini jambo linapokuwa kinyume chake, hapo ndipo maswali mengi yanapoibuka juu ya maendeleo ya mchezaji huyo ndani ya uwanja.

LONDON, ENGLAND: MAISHA yanakwenda kasi si mchezo. Na muda umekuwa na thamani kubwa kwenye soko la wanasoka duniani na kuna wengine mambo yao yanakuwa matamu kwa maana ya thamani zao kupanda huku wengine wakikumbana na vitu vigumu katika msimu jambo linalofanya thamani zao kushuka.

Thamani ya mchezaji kupanda sokoni ni kitu kinachofurahiwa na karibu kila mtu, lakini jambo linapokuwa kinyume chake, hapo ndipo maswali mengi yanapoibuka juu ya maendeleo ya mchezaji huyo ndani ya uwanja.

Kwa mujibu wa Transfermarkt hii hapa orodha ya masupastaa 10, ambao thamani zao zimeshuka kwa kiasi kikubwa sana sokoni.

SOK 10

10) Kylian Mbappe (Real Madrid)

Thamani ya zamani: Euro 180 milioni

Thamani ya sasa: Euro 160 milioni

Kiwango kilichoshuka: Euro 20 milioni

Mwanzo hafifu kwenye klabu yake mpya ya Real Madrid imekuwa na athari kubwa kwenye thamani ya mshambuliaji wa kimataifa wa Ufaransa, Kylian Mbappe. Kwa sasa mkali huyo ameanza kujikongoja akifunga mabao tisa katika mechi tisa za mwisho, lakini bado anajitafuta hajajipata sana kwa kulinganisha na kiwango chake cha zamani alipokuwa Paris Saint-Germain. Thamani ya Mbappe sokoni imeshuka maradufu, kutoka kuwa kwenye orodha ya wanasoka wenye thamani kubwa zaidi sokoni hadi kuwa kwenye mastaa wa viwango vya kawaida na mwanzoni Mbappe thamani yake ilikuwa ikisoma Euro 180 milioni sokoni, lakini hiyo imeshuka kwa Euro 20 milioni na hivyo sasa thamani yake halisi sokoni kwa mujibu wa Transfermarkt ni Euro 160 milioni.

SOK 09

9) Aurelien Tchouameni (Real Madrid)

Thamani ya zamani: Euro 100 milioni

Thamani ya sasa: Euro 80 milioni

Kiwango kilichoshuka: Euro 20 milioni

Kuna nyakati kiungo wa Kifaransa, Aurelien Tchouameni alikuwa akihusishwa na mpango wa kuhama Real Madrid kutokana na kukosa nafasi ya kucheza mara nyingi katika kikosi hicho cha Los Blancos, huku Arsenal na Liverpool zilikuwa zikitajwa kuhitaji saini yake, hilo lilidaiwa kushusha thamani ya kiungo huyo sokoni kwa mujibu wa mtandao wa masuala ya uhamisho na bei za mastaa wa soka huko sokoni. Thamani ya Tchouameni imeripotiwa kushuka kwa Euro 20 milioni kutoka Euro 100 milioni iliyokuwa zamani hadi Euro 80 milioni ya sasa, ambayo inaelezwa, ukilipa kiwango kama hicho kunasa saini yake utakuwa haujapigwa cha juu.

SOK 08

8) Matthijs de Ligt (Man United)

Thamani ya zamani: Euro 65 milioni

Thamani ya sasa: Euro 45 milioni

Kiwango kilichoshuka: Euro 20 milioni

Mambo yake si mabaya sana huko Old Trafford ikiwa ni msimu wake wa kwanza katika kuitumikia miamba ya soka ya Ligi Kuu England, Manchester United. Ni mara yake ya kwanza pia kwa beki huyo wa Kidachi kucheza kwenye Ligi Kuu England, hivyo ni jambo la wazi akakumbana na wakati mgumu katika kuonyesha kiwango chake bora uwanjani, akihitaji kuzoea mazingira kwanza kabla hajaanza kuhukumiwa kutokana na kiwango chake. Wakati De Ligt akiwa anajitafuta kwenye klabu yake mpya huko Man United, thamani yake sokoni inaripotiwa kushuka pia kwa Euro 20 milioni, kutoka Euro 65 milioni kwenye thamani yake ya zamani sokoni hadi ya sasa inayosoma ni Euro 45 milioni kwa mujibu wa Transfermarkt.

SOK 07

7) Gabriel Jesus (Arsenal)

Thamani ya zamani: Euro 65 milioni

Thamani ya sasa: Euro 45 milioni

Kiwango kilichoshuka: Euro 20 milioni

Kushuka thamani yake sokoni kwa mshambuliaji wa Arsenal, Gabriel Jesus inapaswa kumwonea huruma. Staa huyo wa Kibrazili amekuwa akisumbuliwa na majeruhi mara nyingi jambo linalomnyima fursa ya kuonekana uwanjani mara kwa mara na hivyo kuigharimu timu yake. Jesus, alirejea uwanjani baada ya kuwa nje ya uwanja muda mrefu na kuonyesha matumaini makubwa ya kuifanya timu yake kushindania ubingwa kwenye Ligi Kuu England, lakini ghafla mambo yalitibuka na kupata maumivu ya goti yanayomfanya kuwa nje ya uwanja muda mrefu. Hilo limefanya thamani yake sokoni kushuka kwa Euro 20 milioni, kutoka Euro 65 milioni ya zamani hadi sasa kuripotiwa kuwa na thamani ya Euro 45 milioni.

SOK 06

6) Ivan Toney (Al-Ahli)

Thamani ya zamani: Euro 50 milioni

Thamani ya sasa: Euro 28 milioni

Kiwango kilichoshuka: Euro 22 milioni

Kabla ya kutimkia zake Saudi Arabia, straika Ivan Toney alikuwa akihusishwa na klabu kubwa za Ligi Kuu England ikiwamo Manchester United na Arsenal zilikuwa zikifukuzia huduma yake ili imng'oe kutoka Brentford. Chelsea nayo ilikuwa ikipiga hesabu za kumnyakua mshambuliaji huyo wa kati wa kimataifa wa England, lakini mambo yalikuwa tofauti anstaa hiyo ametumkia zake huko Saudia kwenda kujiunga na Al-Ahli. Lakini, baada ya kutua tu huko kwenye Saudi Pro League, ndani ya miezi sita tu, thamani yake sokoni imeshuka kwa Euro 22 milioni kutoka Euro 50 milioni hadi Euro 28 milioni kwa mujibu wa mtandao wa Transfermarkt unavyoripoti thamani ya mchezaji huyo sokoni kwa sasa.

SOK 05

5) Victor Osimhen (Galatasaray)

Thamani ya zamani: Euro 100 milioni

Thamani ya sasa: Euro 75 milioni

Kiwango kilichoshuka: Euro 25 milioni

Napoli iliweka kipengele kwenye mkataba wa straika Victor Osimhen wakati inamtoa kwa mkopo kwenda Galatasaray, itahitaji Euro 75 milioni kwenye mauzo ya mchezaji huyo endapo kama kutakuwa na timu itakayohitaji huduma yake. Osimhen amekwenda Uturuki akiwa kwenye kipindi bora kabisa cha maisha yake ya soka na jambo hilo kwa namna fulani liliporomosha thamani yake sokoni kwa Euro 25 milioni, kutoka Euro 100 milioni hadi Euro 75 milioni. Kwa hali ilivyo, Osimhen atarudi kucheza soka kwenye Ligi Kuu tano bora Ulaya kuanzia msimu ujao baada ya kushindwa kubadili timu kwenye dirisha dogo. Bila shaka saini yake itanaswa na timu vigogo kwenye uhamisho wa dirisha la majira ya kiangazi huko Ulaya.

SOK 03

4) Douglas Luiz (Juventus)

Thamani ya zamani: Euro 70 milioni

Thamani ya sasa: Euro 45 milioni

Kiwango kilichoshuka: Euro 25 milioni

Manchester United iliripotiwa kufanya mchakato wa kutuma ofa ya kumnasa kiungo wa zamani wa Aston Villa, Douglas Luiz dirisha la Januari ili arudi kukipiga kwenye Ligi Kuu England. Staa huyo wa Kibrazili amekuwa na wakati mgumu huko Italia alikokwenda kujiunga katika klabu ya Juventus, ambayo imemfanya aanze kwenye mechi tano tu chini ya kocha Thiago Motta msimu baada ya uhamisho wake wa Pauni 43 milioni kwenye dirisha la majira ya kiangazi la mwaka jana. Kukosa nafasi ya kucheza mara kwa mara kumechangia kushusha thamani ya Luiz huko sokoni kwa Euro 25 milioni kutoka Euro 70 milioni hadi thamani yake ya sasa ya Euro 45 milioni kwa mujibu wa mtandao wa Transfermarkt.

SOK 02

3) Frenkie de Jong (Barcelona)

Thamani ya zamani: Euro 70 milioni

Thamani ya sasa: Euro 45 milioni

Kiwango kilichoshuka: Euro 25 milioni

Ilishangaza kuona hakukuwa na uvumi mwingi wa kuhusiana na Manchester United kwenye dirisha la Januari kwa kiungo wa Kidachi, Frenkie de Jong. Kwa miaka kadhaa sasa kila kinapofika kipindi cha usajili, De Jong amekuwa akihusishwa na miamba ya soka ya Old Trafford na bila shaka jambo hilo litakwenda kutokea tena kwenye dirisha lijalo la majira ya kiangazi hasa baada ya kuripotiwa kwamba Barcelona ipo tayari kumfungulia mlango wa kutokea staa huyo.

Majeraha na kushindwa kupata nafasi ya kucheza mara kwa mara kumeripotiwa kushusha thamani ya De Jong kwa Euro 25 milioni huko sokoni kutoka Euro 70 milioni hadi Euro 45 milioni, huku ikielezwa itakapofika mwisho wa msimu, mkataba wake utakuwa umebakiza mwaka mmoja.

SOK 01

2) Leroy Sane (Bayern Munich)

Thamani ya zamani: Euro 70 milioni

Thamani ya sasa: Euro 45 milioni

Kiwango kilichoshuka: Euro 25 milioni

Kuwasili kwa winga Michael Olise huko Bayern Munich kumemfanya Leroy Sane kupoteza nafasi yake ya kuanza kwenye kila mechi katika kikosi hicho cha kocha Vincent Kompany. Na sasa mambo yalivyo, winga huyo wa Ujerumani anaweza kuachana na Bayern Munich mwishoni mwa msimu huu wakati mkataba wake utakapofika tamati. Kitu kizuri kwa Sane ni kwamba hatakosa timu za kwenda kujiunga nazo itakapofika mwisho wa msimu kutokana na kile ambacho bado anaweza kukifanya ndani ya uwanja. Lakini, kutokana na kukosa nafasi ya kucheza na mkataba wake kuelekea ukingoni hilo limeshusha thamani ya Sane sokoni kwa Euro 25 milioni, kutoka Euro 70 milioni hadi Euro 45 milioni.


SOK 04
SOK 04

1) Lucas Paqueta (West Ham)

Thamani ya zamani: Euro 65 milioni

Thamani ya sasa: Euro 40 milioni

Kiwango kilichoshuka: Euro 25 milioni

Ni wazi kabisa, kiungo wa Kibrazili, Lucas Paqueta kwa sasa angekuwa anakipiga kwenye kikosi cha Manchester City, tena ambayo ingekuwa imemsajili kwa pesa nyingi sana isiyopungua Pauni 100 milioni kama si jina lake kuhusishwa kwenye ishu ya kubeti na kumtibulia maisha yake kwenye mchezo wa soka. Mambo kama hayo yamemtibulia kwa kiasi kikubwa thamani ya Paqueta sokoni na imeshuka kwa Euro 25 milioni kutoka Euro 65 milioni hadi Euro 40 milioni inayotajwa kwa sasa na mtandao wa Transfermarkt. Kama kuna vipaji matata kabisa kwenye mchezo wa soka basi kimoja wapo ni hiki cha Paqueta, lakini mambo ya kubeti yametibua mambo mengi ya kumwaandikia sifa mbaya mchezaji huyo.