Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Nado: Kwa Azam hii, hakuna kinachoshindikana

NADO Pict

Muktasari:

  • Nado aliisaidia Azam kutinga hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho akipiga mabao mawili dhidi ya KMKM katika mchezo wa marudiano ikishinda 7-0 kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, jijini Dar es Salaam, baada ya awali kushinda 2-0 visiwani Zanzibar na Wanalambalamba hao kuweka historia ya kufuzu kwa mara ya kwanza tangu ianze kushiriki michuano hiyo.

INAWEZEKANA. Ndivyo anavyosema winga wa Azam FC, Iddi Seleman 'Nado' ambaye msimu huu anauona wakifanya vizuri na suala la ubingwa kwao ni kukaza tu, hawashindwi.


Nado aliisaidia Azam kutinga hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika akipiga mabao mawili dhidi ya KMKM katika mechi ya marudiano ikishinda 7-0 kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi jijini Dar es Salaam, baada ya awali kushinda 2-0 visiwani Zanzibar na Wanalambalamba hao kuweka historia ya kufuzu kwa mara ya kwanza tangu ianze kushiriki michuano hiyo.

Nado amepiga stori na Mwanaspoti na analiambia mambo mbalimbali ikiwamo ndoto ya kubeba mataji ikiwamo la Ligi Kuu Bara msimu huu.

NAD 01

UBINGWA LIGI KUU

Hii ni ndoto ya kila mchezaji wa Ligi Kuu ya nchi yoyote. Hapa nchini katika Ligi Kuu Bara, nyota wengi wanatamani kufikia mafanikio hayo na wengi hutamani kucheza vikosi vya Yanga na Simba ambavyo vina uhakika wa kubeba mataji.

Hata hivyo, kwa Nado ambaye alijiunga na Azam FC akitokea Mbeya City mwaka 2019 na hajawahi kunyanyua kwapa kutwaa taji hilo kubwa nchini, anasema analitamani sana kwa sababu mengine na hasa ya Ndondo kabeba sana.

“Mimi nimeibukia katika soka la mtaani na nimecheza Ndodo Cup. Huko nimebeba sana nikiwa Manzese. Kwa sasa nataka kombe la Ligi Kuu Bara,” anasema na kuongeza;

“Nimecheza ligi kuu kwa misimu mingi sasa, ndoto yangu ni kuona nabeba taji. Hata kama haitatokea hivyo, basi hata la Shirikisho. Naamini inawezekana. Hakuna kinachoshindikana.”

NAD 03

MAKUNDI NI MWANZO TU

Anasema kwa kikosi walichonacho msimu huu, anatamani kuona wanafika mbali zaidi ya walipo (makundi) na wapo tayari kupambana, akiweka wazi pia anatamani kufunga mabao zaidi kuisaidia timu yake na zaidi mabao bora.

“Azam FC ni timu kubwa kuishia makundi siyo mwisho, natamani kuona tunafika fainali ya michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika. Kutinga makundi ni mwanzo mzuri bado tuna nafasi ya kufanya vizuri zaidi,” anasema na kuongeza;

“Furaha yangu kubwa ni kufunga mabao na sio mabao tu, bali mazuri na ndiyo maana nipofunga dhidi ya KMKM  nilishangilia kwa furaha sana.”

NAD 05

WINGA MBIO

Mmoja wa wachezaji wenye kasi katika Ligi Kuu Bara ni Nado na anasema ni moja ya mambo yanayowasaidia mawinga wengi kuwa na ubora.

Anasema kasi yake inamsaidia kuwa na kiwango kizuri na kuisaidia timu yake katika kufunga mabao na kutoa pasi za mwisho au kutengeneza nafasi.

“Usipokuwa na kasi huwezi kufika kwa wakati maeneo sahihi, kucheza winga na beki ya kushoto au kulia unatakiwa kuwa na kasi ili kufika kwenye maeneo kwa wakati na ndio maana unaona nakimbia sana,” anasema na kuongeza;

“Nafasi ninayocheza naifurahia na imekuwa ikinipa nafasi ya kufanya yale ninayoyafanya, pia nikiwa kama winga kitu pekee ninachokifurahia ni kufunga, napenda sana kufunga kuliko kutengeneza.”

NAD 04

BAO BORA

Amefunga mabao mengi sana akiwa na Azam FC, lakini hapa analitaja bao lake dhidi ya Simba katika sare ya  2-2, ndilo bora tangu aanze kucheza soka la ushindani na alimtungua kipa Aishi Manula.

Anasema mechi hiyo ilichezwa Februari 10, 2021 na mabao ya Simba yalifungwa na Meddie Kagere na Luis Misqussone huku ya Azam FC yakifungwa na yeye mwenyewe, huku la pili likifungwa na Ayub Lyanga na pasi ya bao ilitoka kwake.

“Nilimfunga Aishi Manula akiwa Simba. Nikiwa nje ya 18 nilipiga shuti kwa mguu wa kushoto. Nimekuwa nikimtesa hadi leo kwa sababu bado namtania.”

“Nimemfunga rafiki yangu, dharau kidogo zimepungua maana sasa tunacheza timu moja na tunakaa karibu wakati wa kula. Kuna muda hata mazoezini nikimpigia mpira ananitania hilo shuti la kike na mimi namkumbushia bao langu bora kuwa ile shuti lilikuwa la kiume siyo.”

NAD 02

FOBA, JOB, DUCHU WAKALI WA MITUPIO

Kwenye soka la Tanzania ukiondoa ubora wa uwanjani Nado amekuwa bora nje ya uwanja kwenye masuala ya kutupia (kuvaa). Pia anavutiwa na namna nyota wenzake baadhi wanavyovaa.

“Mimi sio mpangiliaji sana kwenye kuvaa, lakini nikivaa huwa nasifiwa nimependeza. Kuhusu kuchagua nguo, huwa nazingatia mazingira ya ninapokwenda ndiyo nijue ipi itanipendeza,” anasema na kuongeza;

“Pia kuna wachezaji wakivaa wanavutia katika kikosi cha Azam akiwamo Zubery Foba, Teps Evans, Yahya Zayd, Pascal Msindo, Lusajo Mwaikenda na wengine, hao ni mfano tu.”

“Nje ya timu yangu Simba kuna David Kameta ‘Duchu’, Dickson Job, Nickson Kibabage, Aboutwarib Mshery hawa pia wanajua sana kuvaa na wanajua kupangilia mavazi.”

NAD 06

ALIPOANZIA

Winga huyu alianza kufahamika zaidi katika mashindano ya mtaani maarufu kama ‘Ndondo Cup’ 2015 wakati huo akiwa anaichezea Makumba FC ya Ilala.

Makumba ni timu ya wauza vifaa vya magari na katika msimu huo, Nado aliiongoza kushika nafasi ya tatu, huku akiibuka mchezaji bora wa mashindano ya Ndondo Cup mwaka huo.

Mwaka 2016 alihamia Misosi FC iliyokuwa na makazi yake mitaa ya Tandale na ilifika hatua ya nusu fainali na kucheza mechi ya kuwania nafasi ya tatu walikofungwa na Makumba FC mechi ambayo Nado hakucheza.

Sababu ya kutocheza ni kujisikia vibaya kucheza dhidi ya timu ambayo msimu mmoja nyuma ilimpa nafasi na kuwa mchezaji bora wa mashindano.

Msimu wa 2017 alicheza tena Misosi FC na safari hii aliiongoza kuwa mabingwa wa michuano hiyo na baada ya msimu huo kwisha alisajiliwa na Mbeya City kwa ajili ya msimu wa Ligi Kuu Bara 2017/18.