Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Maseke: Kutoka Bunda hadi kikosi cha kwanza JKT Queens

MASEKE Pict

Muktasari:

  • Maseke katika muda mfupi ameibuka kuwa mmoja wa mabeki wanaoaminika zaidi kwenye soka la wanawake nchini.

UKITAJA listi ya mabeki bora kwenye Ligi ya Wanawake msimu uliomalizika basi lazima jina la Ester Maseke liwepo kutokana na ubora aliouonyesha ndani ya msimu wake wa kwanza akiwa na kikosi cha JKT Queens.

Maseke katika muda mfupi ameibuka kuwa mmoja wa mabeki wanaoaminika zaidi kwenye soka la wanawake nchini.

Safari yake ya mafanikio ilianzia Bunda Queens chini ya Kocha Alley Ibrahim. Wakati huo Maseke hakuwa beki kama wengi wanavyomfahamu sasa, bali alikuwa kiungo mkabaji aliyekuwa akiongoza eneo la kati kwa utulivu na nidhamu kubwa.

Kiwango chake kilimfanya awe miongoni mwa wachezaji wa kwanza kuanza kikosini karibu kila mechi kutokana na ubora aliokuwa akiouonyesha.

Ubora aliouonyesha akiwa na JKT Queens ulimfanya abebe tuzo ya mchezaji bora chipukizi kwa wanawake msimu uliopita.

Mwanaspoti limekuchambulia safari ya nyota huyo ambaye usajili wake haukuimbwa sana lakini amekuwa mhimili mkubwa kwenye safu ya beki ya JKT.

MASE 01

BUNDA HADI JKT

Baada ya kuonyesha ubora mkubwa ulimvutia kocha wa JKT wakati huo inafundishwa na Ester Chabruma aliyemvuta kikosini hapo.

Hata hivyo, kabla ya kujiunga na Wanajeshi hao wa kike, kocha wa timu ya taifa, Twiga Stars, Bakari Shime alipomuita kwa mara ya kwanza alimtumia kama beki wa kati badala ya kiungo kama ilivyozoeleka.

Tangu hapo hadi JKT imekuwa ikimtumia kwenye nafasi hiyo akicheza vizuri na kuelewana na mkongwe Anastazia Katunzi ambaye naye anamudu kucheza nafasi mbalimbali ikiwemo beki wa pembeni.

Inaelezwa hata uhamisho wake kwenda JKT Queens, Shime ambaye alikuwa akimfuatilia kwa karibu akiwa Bunda Queens, ndiye aliyependekeza asajiliwe baada ya kuvutiwa na uwezo wake katika mechi mbalimbali za ligi.

Kabla ya kujiunga na JKT ilikuwa ikiwatumia Christer Bahera, Happyness Mwaipaja na Katunzi kwenye eneo la beki wa kati, lakini tangu amefika amelidumu eneo hilo vizuri na kuchukua nafasi moja kwa moja.

MASE 05

TWIGA STARS

Ubora huo haukuishia tu kwenye ligi hadi kwenye timu ya taifa tangu apewe nafasi na kocha Shime amekuwa akitumia vizuri.

Twiga Stars ina nyota wengi kwenye eneo la beki wa kati Noela Luhala, Juleitha Singano, Violeth Nickolaus, Ester Mayala, Anastazia Katunzi na wengineo.

Wachezaji hao walikuwa wakipewa nafasi ya kuanza kutokana na uzoefu na kiwango walichokuwa wakikionyesha kwa muda mrefu.

Lakini mambo yakaanza kubadilika baada ya Maseke kuendelea kung’ara akiwa na jezi ya JKT.

Kiwango chake kilimfanya Shime asiwe na sababu ya kumuacha nje ya kikosi na taratibu akaanza kujitengenezea nafasi ya kudumu kwenye timu ya taifa.

MASE 02

Hivi sasa kila Twiga Stars inapoitwa kambini, jina la Maseke limekuwa miongoni mwa ambayo hayakosekani. Amejenga imani kubwa kwa benchi la ufundi kutokana na uwezo wake wa kusoma mchezo, kucheza kwa utulivu na kuongoza safu ya ulinzi katika mechi zenye presha kubwa.

Moja ya vitu vilivyomsaidia zaidi ni kucheza sambamba na Anastazia Katunzi ndani ya JKT Queens. Uelewano walioujenga klabuni umehamia pia kwenye kikosi cha Twiga Stars, jambo ambalo limeifanya safu ya ulinzi ya timu ya taifa kuwa imara zaidi.

Wawili hao wamekuwa wakielewana kwa urahisi, wakisaidiana katika kuzuia mashambulizi na kuipa timu utulivu inapokuwa chini ya presha.

MASE 03 (1)

KIMATAIFA

Msimu uliopita JKT ilicheza mashindano ya Ligi ya Mabingwa huko pia Maseke alikiwasha  hadi kunyakuwa tuzo ya mchezaji bora wa mechi dhidi ya Asec Mimosas ya Ivory Coast.

Kwenye mashindano hayo Maseke alionyesha kiwango bora licha ya JKT Queens kumaliza kundi B ikiwa na pointi mbili.

Maseke aliingia kwenye orodha ya wateule wa tuzo ya mchezaji bora chipukizi wa mwaka tuzo zilizokuwa zinazotolewa na Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF).

MASE 03

WASIKIE WADAU

Kocha wa Bunda, Alley Ibrahim “Kwanza ni mchezaji mwenye nidhamu kubwa ndani na nje ya uwanja naamini ana uwezo mkubwa na naamini ataendeleza ubora wake.”