Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mambo 10 yanayoharibu muonekano wako hata ukivaa nguo nzuri

Muktasari:

  • Unaweza kuvaa nguo ya gharama, ya kisasa na inayokufaa, lakini bado ukapoteza mvuto wako kwa sababu ya vitu vidogo vinavyoonekana vya kawaida lakini vina athari kubwa kwenye taswira yako.

Kuna watu wanapojitokeza, unashindwa kuelewa kama tatizo ni nguo au kitu kingine kinachoharibu picha yao kwa ujumla. Ukweli ni kwamba mwonekano mzuri hauishii kwenye mavazi pekee.

Unaweza kuvaa nguo ya gharama, ya kisasa na inayokufaa, lakini bado ukapoteza mvuto wako kwa sababu ya vitu vidogo vinavyoonekana vya kawaida lakini vina athari kubwa kwenye taswira yako.

Mwonekano wa mtu ni mchanganyiko wa usafi, mpangilio, umbo la mwili na namna anavyojihudumia kwa jumla. Makala hii inaangazia vitu vidogo ambavyo mara nyingi watu huyapuuzia, lakini vinavyoweza kuharibu kabisa mvuto wa mavazi mazuri.


USAFI WA MWILI

Kwanza kabisa ni usafi wa mwili na harufu ya mwili. Hii ni moja ya mambo yanayoweza kuharibu kila kitu. Unaweza kuvaa suti nzuri au gauni la kifahari, lakini kama hujajisafisha vizuri au unatoa harufu mbaya ya mwili (kikwapa), watu wataona tatizo kabla ya kuona mavazi yako. Usafi wa mwili, kuoga mara kwa mara, kutumia 'deodorant' na kuhakikisha mwili wako uko safi ni msingi wa muonekano mzuri.


RANGI YA VIATU

Viatu visivyo na mpangilio mzuri wa rangu. Watu wengi huangalia mavazi kuanzia juu, lakini macho hushuka moja kwa moja hadi kwenye viatu. Viatu vilivyochakaa au visivyo na rangi ya kuvutia yenye utulivu vinaweza kuvuruga kabisa muonekano wako. Hata kama umevaa nguo nzuri kiasi gani, viatu vibovu vitakupunguzia hadhi mara moja.

KUPIGA PASI

Nguo zisizopigwa pasi au zisizo na umakini wa uvaaji. Nguo zilizokunjamana, zilizo na doa au zisizokaa vizuri mwilini huonyesha uzembe. Wakati mwingine mtu anaweza kuwa na nguo nzuri lakini akashindwa kuonekana vizuri kwa sababu hajazingatia pasi au mpangilio wa uvaaji. Nguo nzuri zinahitaji heshima yake ili zitoe matokeo mazuri.


MITINDO YA NYWELE

Nywele na ndevu zisizotunzwa. Nywele zisizopangwa, ndevu zisizopunguzwa au mtindo usio mzuri unaweza kuharibu kabisa sura ya mtu. Nywele ni sehemu ya kwanza ya uso wa mtu na zina nafasi kubwa katika kuonyesha usafi, unakutana na mtu kapendeza lakini kavaa wigi baya au kasuka mtindo mzuri ila kachanganya rangi, wakati mwingine nywele vimefumuka mpaka zimechakaa kabisa.


KUCHA CHAFU

Kucha chafu au ndefu kupitiliaza, Watu wengi hufikiria mavazi pekee, lakini mikono ni sehemu inayoonekana sana hasa unapoongea au kusalimiana.

KURUDIA NGUO BILA KUFUA

Harufu ya mavazi (nguo zisizo safi au zilizojaa jasho). Nguo zinaweza kuwa safi kwa macho lakini kama zimevaliwa mara nyingi bila kufuliwa vizuri au zina harufu ya jasho, zinapoteza thamani yake. Harufu mbaya kwenye nguo inaweza kumfanya mtu apoteze heshima hata kabla hajaanza kuzungumza.


KUPANIA SANA

Kupitiliza mapambo au kutumia vifaa visivyoendana. Watu wengine huvaa saa kubwa sana, miwani isiyoendana, mikufu mingi au mapambo yasiyo na mpangilio. Badala ya kuongeza mvuto, huweza kuharibu uhalisia wa muonekano. Urembo mzuri ni ule wenye uwiano na umakini, si uwingi wa vitu.


MWENDO

Lugha ya mwili (body language). Mtu anaweza kuvaa vizuri lakini akitembea kwa kutojiamini, mabega yameinama au uso hauna tabasamu, muonekano wake unapoteza nguvu. Lugha ya mwili inaongeza au kupunguza thamani ya mavazi yako bila hata kusema neno.


MUONEKANO UENDANE NA MAHALI

Kutokuzingatia umri na mahali unapokwenda. Kuna watu huvaa nguo nzuri lakini zisizoendana na mazingira. Mavazi ya kilichopo klabu si lazima yafanane na ya kazini au kwenye hafla rasmi. Kutokulinganisha mavazi na mazingira huweza kuharibu taswira yako.

KUTOKUJIAMINI

Mwisho ni kutokujiamini. Hili ni jambo la ndani lakini linaonekana nje. Mtu anaweza kuvaa vizuri lakini akiwa hana kujiamini, anaonekana vibaya. Kujiamini kunakamilisha muonekano mzuri na kuufanya uwe na nguvu zaidi.


USHAURI

Kama unataka kuonekana wa kipekee na mwenye mvuto wa kweli, zingatia vitu vidogo. Ndiyo vinavyotengeneza tofauti kati ya mtu anayeonekana wa kawaida na yule anayevutia kwa mara ya kwanza sio nguo nzuri pekee.