Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kwa mziki wa Winfrida, Mukandayisenga ngoja tuone itakuwaje

JKT Pict

Muktasari:

  • JKT imeweka rekodi ya kuwa timu ya kwanza kuchukua ubingwa huo mara mbili mfululizo; mwaka jana iliichapa Yanga Princess bao 1-0, na mwaka huu ikanyakua tena mbele ya pacha mwingine wa Kariakoo Simba.

JKT Queens imeandika historia kwa kutwaa ubingwa wa Ngao ya Jamii kwa Wanawake baada ya kuifunga Simba Queens mabao 2-1, lakini nyuma yake kuna mambo kibao yamebaki rekodi.

Timu hiyo imeweka rekodi kuwa ya kwanza kuchukua ngao mara mbili mfululizo; mwaka jana iliichapa Yanga Princess bao 1-0 na huu ikiinyakua tena mbele ya pacha mwingine wa Kariakoo, Simba.

Rekodi ya pili ni kuwa timu ya kwanza kucheza fainali zote tatu tangu mashindano hayo yaanze 2023, ambapo Simba ilikuwa mabingwa wa kwanza kisha ikafuata JKT kwa misimu miwili mfululizo.

JK 05

Rekodi nyingine ni kuwa JKT yenye nyota wengi wazawa imechukua ubingwa mbele ya vigogo Simba Queens na Yanga Princess. Msimu huu imezifunga timu zote mbili  Yanga ikiwatoa kwa penalti katika nusu fainali na Simba ikawapiga 2-1 kwenye fainali. Lakini, achana na rekodi hizo kuna nyota waliovutia na kujizolea sifa kutoka kwa mashabiki.

JK 01

WINIFRIDA GERALD

Katika safu ya ushambuliaji ya JKT jina la Winifrida Gerald lilitawala. Binti huyo alionyesha kiwango bora akicheza soka la kisasa akiwa na uelewa wa kuwasoma wapinzani na wakati sahihi wa kuanzisha mashambulizi yaliyozaa matunda.

Winifrida hakuonesha tu umahiri wa kiufundi, bali pia kujiamini na utulivu wa hali ya juu  sifa zilizomfanya kutangazwa rasmi kuwa Mchezaji Bora wa Mashindano (MVP). Alikuwa injini ya timu, daraja kati ya kiungo mshambuliaji na safu ya ushambuliaji. Aling’ara kwenye mechi zote dhidi ya Simba Queens na Yanga Princess. Si jambo geni kwake, kwani hata kabla ya kujiunga na kikosi hicho cha Kujenga Taifa alikuwa na jina kubwa.

Uwezo wake wa kupokea pasi, kukaa na mpira mguuni, kuangalia wapi pa kupenya na kuwazidi maarifa mabeki wa timu pinzani, uliwaumiza mabeki wengi wa Ligi Kuu wakimtaja kama mwiba mchungu. Si mchezaji wa maneno mengi, lakini kila aliyeshuhudia mashindano kuanzia nusu fainali hadi fainali, aliondoka na jina lake kichwani – kinda anayekuja kwa kasi.

Aliwahi kuibuka mchezaji bora kwenye mashindano ya African School, na MVP kwenye CAF U-17 Girls Integrated Football Tournament (GIFT). Huu ni muendelezo wa kiwango chake bora.

JK 02

JEANINE MUKANDAYISENGA

Achana na tuzo ya mfungaji bora wa mashindano dakika 180 za mashindano hayo zilitosha kuonyesha ubora wake. Kasi, nguvu, utulivu, na namna ya kumalizia pasi za viungo ni baadhi ya sifa zake. Uwepo wake ndani ya eneo la hatari ulikuwa tishio kwa safu yoyote ya ulinzi. Alijua lini atoe pasi, lini asubiri mpira, na alikuwa na karibu kila sifa ya namba 9 halisi.

Alifunga mabao mawili: moja kwenye nusu fainali dhidi ya JKT (ambapo walienda sare 1-1 kabla ya kupigwa penalti), na moja kwenye mechi ya mshindi wa tatu dhidi ya Mashujaa alitoa pia asisti mbili.

Uwezo wake wa kulazimisha kuvunja ukuta wa wapinzani ni tishio, kiasi cha mashabiki kuanza kumtabiria kuwa mfungaji bora wa msimu ujao. Msimu uliopita, akiwa mchezaji wa dirisha dogo, alifunga mabao 12 kwenye mechi tisa kama akiendeleza kiwango chake, ana nafasi kubwa ya kuwa mfungaji bora wa ligi.

JK 03

SIMBA, YANGA BADO

Ukiachana na viwango vya wachezaji mmoja mmoja, Simba na Yanga bado zinaonekana kuwa na changamoto kulingana na mechi walizocheza kwenye mashindano hayo – ambayo yanatoa taswira ya maandalizi kuelekea msimu mpya wa ligi.

Simba, iliyoingiza wachezaji wapya zaidi ya 13, bado haina muunganiko. Wengi wanaonekana na changamoto ya fitinesi na uzito wa kufanya maamuzi ya haraka – tofauti na timu zingine.

Hata hivyo, kwa upande wa wachezaji mmoja mmoja, baadhi walionyesha ubora – hasa kipa Ruth Aturo, ambaye licha ya kufungwa mabao mawili yaliyotokana na upungufu wa ulinzi alicheza kwa utulivu na kuanzisha mashambulizi kutoka nyuma.

Brice Zanga, kiungo kutoka Cameroon aliyejiunga kipindi cha dirisha kubwa alionyesha kiwango bora. Hapo awali alikuwa beki wa kushoto, lakini alitumika kama kiungo mzuiaji na akaongoza mashambulizi kama namba sita huru.

Kwa upande wa Yanga, changamoto iko kwenye umaliziaji. Mukandayisenga akiwa na mpira au kwenye muvi mara nyingi hukosa msaada kutoka kwa mawinga au viungo washambuliaji kama Aregash Kalsa na Precious Christopher.

Ndiyo maana pasi nyingi alizopewa ziliishia kupotea, au kuingiliwa kutokana na kukosa msaada wa haraka.

Hata hivyo, kuna maendeleo - usajili wa kiungo Ritticia Nabbosa na beki Ester Akudo umeongeza uimara. Akudo ana uwezo wa kukaba mipira ya juu na chini, mtu kwa mtu, na kutoa pasi kwa usahihi.

Safu ya ulinzi ya Yanga inaonekana kuimarika zaidi - Akudo, Igwe Uzoamaka na Angela Chineneri wamekuwa wakicheza kwa kuelewana. Igwe na Angela wamekuwa pamoja tangu msimu uliopita, lakini ujio wa Akudo umeleta kitu zaidi  ni beki mwenye akili, matumizi bora ya mwili na miguu, na uwezo wa kuanzisha mashambulizi.

JK 04

JKT QUEENS

Ni timu yenye kikosi finyu lakini hucheza kwa kubadilika kulingana na mechi. Tofauti ya mashindano ya Cecafa nchini Kenya na Ngao ya Jamii ilionekana wazi.

Mechi ya kwanza dhidi ya Yanga Princess walicheza chini ya kiwango, hasa eneo la kiungo – Donisia Minja alipoteza pasi nyingi kwa upande wa Winifrida na Stumai Abdallah. Lakini kwenye fainali walibadilika. Kocha Kessy Abdallah alitumia mfumo wa 4-3-3  uliomwezesha kushambulia kwa kasi huku akiweka uwiano kwenye ulinzi, kiungo na ushambuliaji.

Aliwatumia mabeki Christer Bahera na Ester Maseke kuhakikisha lango lipo salama, huku Janeth Pangamwene (namba 6), Elizabeth Chenge (namba 8) na Donisia Minja wakicheza kama viungo watatu. Viungo hao waliunganisha safu ya ulinzi na ushambuliaji, kugawa pasi na kushambulia kwa utulivu. Katika ushambuliaji, alitumia Winifrida, Jamila Rajabu na Stumai Abdallah walivuruga sana safu ya ulinzi ya Simba.

JKT Queens walitawala mechi kuanzia mwanzo hadi dakika ya 75 kwa pressing ya hali ya juu, umiliki wa mpira na kasi ya kushambulia  hali iliyowafanya Simba kucheza kwa kutoelewana.