Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kocha Serengeti Boys aendelezwe kitaaluma

SERENGETI Pict

Muktasari:

  • Sasa wanapotokea makocha wazawa ambao wanaonyesha wana kitu spesho na wana uthubutu wa kupiga hatua kubwa zaidi, tunaamini wanapaswa kutiwa moyo na kuhamasishwa ili wafike juu zaidi.

IKO wazi Tanzania tuna makocha wengi wa soka lakini wale wa daraja la juu wa kuweza kushindana kimataifa ni wachache.

Huo ndiyo ukweli mchungu ambao tumekubaliana hapa kijiweni hivyo atakayeupokea sawa na ambaye hatoupokea pia sawa vilevile.

Sasa wanapotokea makocha wazawa ambao wanaonyesha wana kitu spesho na wana uthubutu wa kupiga hatua kubwa zaidi, tunaamini wanapaswa kutiwa moyo na kuhamasishwa ili wafike juu zaidi.

Mfano wa hao ni Kocha Elieneza Nsanganzelu ambaye hivi karibuni ametoka kuiongoza Serengeti Boys kufanya mambo makubwa katika Fainali za Mataifa ya Afrika kwa Vijana chini ya umri wa miaka 17.

Kwa mara ya kwanza katika historia, madogo wameingia katika fainali jambo ambalo halikuwahi kufanywa na timu yoyote ya taifa hapa Tanzania katika fainali za AFCON lakini pia wamefanikiwa kufuzu Kombe la Dunia.

Hawajafanya hayo kwa bahati mbaya bali wameonyesha soka safi, la kuvutia na la kufundishwa, jambo ambalo ni matokeo ya kazi nzuri iliyofanywa na benchi la ufundi lililo chini ya Kocha Nsanganzelu.

Sasa inabidi tuwekeze kwa huyu kocha na ikibidi na wasaidizi wake ili waendelee kututengenezea wachezaji bora vijana ambao watakuwa chachu ya mafanikio kisoka kwa taifa letu siku za usoni.

Yeye na wanaomsaidia wapewe sapoti ya kusoma kozi toshelezi za ukocha na utawala ambazo zitawajenga na kuwaimarisha zaidi katika taaluma yao hiyo.

Hiyo itasaidia kuhamasisha wengine kujituma na kuonyesha uthubutu zaidi kwa vile wataona wakifanya vizuri wanathaminiwa tofauti na dhana makocha wazawa wanadharaulika.