Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kismati cha kina Loemba, Depu CAF

KISMAT Pict


SIMBA, Yanga, Azam na Singida Black Stars zinapishana viwanja tu katika michuano ya kimataifa, zikiwa ndizo timu nne zinazoiwakilisha nchi kwa sasa.


Simba na Yanga zinashiriki Ligi ya Mabingwa Afrika, wakati Azam FC na Singida Black Stars zikiwa Kombe la Shirikisho Afrika.


Timu hizo zote nne bado zina nafasi ya kupambania kufuzu robo fainali, huku kila moja ikiwa imebakiwa na mechi tatu.

Ni Simba pekee kati ya zote ambayo haijakusanya pointi hata moja kwenye kundi lake.

Licha ya Simba kutokusanya pointi hata moja katika mechi tatu ilizocheza, bado ina nafasi ya kutinga hatua ya robo fainali endapo itapata ushindi katika mechi tatu zilizobaki na kufikisha pointi tisa, huku ikiomba wapinzani wake wateleze.

Achana na hayo, kupitia nafasi za uwakilishi wa timu hizo nne kimataifa, kuna nyota ambao wamepata fursa ya kucheza michuano ya kimataifa bila matarajio, baada ya kutua katika timu hizo kipindi cha dirisha dogo la usajili.

Mwanaspoti linakuletea baadhi ya wachezaji hao kutoka timu za Simba, Yanga, Azam na Singida Black Stars, timu ambazo zitakuwa na kibarua wikiendi hii katika viwanja tofauti.

KISM 04

EMMANUEL MWANENGO

Alikuwa mchezaji wa kwanza kutambulishwa Yanga, akiwa amesajiliwa akitokea Tabora United, ambayo kwa sasa ni TRA United.

Nyota huyo tayari amevaa medali ya Kombe la Mapinduzi 2026, akiwa sehemu ya wachezaji waliopambania taji hilo kwa kuifunga Azam kwa penalti 5-4.

Mwanengo imekuwa bahati kwake kuvaa medali, lakini pia kuwa mmoja wa wachezaji wanaoiwakilisha Yanga katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, kwani timu aliyotoka haikuwa sehemu ya timu zinazowakilisha kimataifa.

KISM 01

ABDULMALICK ZAKARIA

Amejiunga na Singida Black Stars akitokea Mashujaa. Tayari amepata nafasi ya kuanza kikosi cha kwanza cha timu hiyo na kucheza mechi za kimataifa, na Singida Black Stars inashiriki Kombe la Shirikisho Afrika, kundi C.

Beki huyo wa kati hakutarajia msimu huu kushiriki michuano hiyo, kwani ametokea Mashujaa, lakini usajili wake ndani ya Singida Black Stars umefanikisha jambo hilo.

KISM 05

ABDALLAH SAID ‘LANSO’

Alianza kucheza Ligi Kuu Bara akiwa na KMC akitokea Mlandege. Akaitumikia KMC kwa msimu mmoja na nusu, na sasa anakipiga Singida Black Stars, iliyompa nafasi ya kushiriki michuano ya kimataifa.

Lanso amejiunga na Singida Black Stars katika dirisha dogo la usajili akiwa mchezaji huru, baada ya kumalizana na KMC.

Beki huyo tayari ameanza kucheza michuano ya kimataifa, akiingia dhidi ya AS Otoho.

KISM 03

MIRAJI ABDALLAH

Ni beki wa pembeni ambaye alianza kuitumikia Coastal Union kabla ya kutua Dodoma Jiji, ambayo ameichezea kwa takriban miezi sita, kisha katika dirisha dogo akasajiliwa na Singida Black Stars. Kwa sasa yupo Congo Brazzaville, tayari kwa mechi ya nne ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya AS Otoho.

Beki huyo, ambaye alitambulishwa saa chache kabla ya kusafiri kuelekea kwenye mchezo huo unaotarajiwa kupigwa Februari Mosi mwaka huu, ni kama zawadi kwake kuongeza uzoefu wa kimataifa, kwani amejiunga na timu inayopambania kusonga hatua ya robo fainali.

KISM 06

ALAIN ANICET

Simba imekamilisha usajili wa Alain Anicet Oura kutoka IF Gnistan ya Ligi Daraja la Kwanza Finland. Ana uwezo wa kucheza winga wa kulia na kushoto, hivyo ni sehemu ya ongezeko la ushindani kwenye namba mbele ya Elie Mpanzu na Kibu Denis.

Oura inaelezwa kuwahi kufanya kazi na kocha Steve Barker wakiwa Stellenbosch, na ni pendekezo lake kusajiliwa katika kikosi hicho. Hivyo, ubora wake utaamua kumweka benchi Mpanzu au Kibu, ambao hata hivyo hawana namba nzuri kikosini msimu huu.

KISM 09

INNO JOSPIN LOEMBA

Ni kiungo mshambuliaji namba 10, mwenye umri wa miaka 22, raia wa Congo Brazzaville, akitokea Colombe Sportive ya Cameroon, naye tayari ni Mnyama.

Hii ni vita nyingine ya namba katika nafasi ya Clatous Chama. Utofauti wao ni uzoefu, huku ubora ukisubiriwa kuamuliwa na muda mara baada ya kila mmoja kupata nafasi.

Kiungo huyo, ambaye anatajwa kwa ufundi katika eneo la ushambuliaji, inaelezwa amejiunga na Simba kwa mkataba wa miaka miwili, na wanaamini ni mchezaji atakayoongeza kitu katika kikosi, akitajwa kuwa na kasi na ubunifu karibu na lango la mpinzani.

KISM 02

LIBASSE GUEYE

Gueye (22) amejiunga na Simba akitokea Teungueth ya Senegal kwa mkataba wa miaka miwili na nusu, ambao utafikia tamati Juni 2028.

Mchezaji huyo anamudu kucheza nafasi tofauti uwanjani na mbali na kiungo mshambuliaji, pia anaweza kucheza kama winga.

Kiwango bora alichokionyesha katika Fainali za Mataifa ya Afrika kwa Wachezaji wa Ligi za Ndani (CHAN) 2024 kimeonekana kuchangia kwa kiasi kikubwa kuishawishi Simba kumnasa nyota huyo.

Gueye ni mchezaji mwenye kasi na uwezo mkubwa wa kutengeneza nafasi za mabao. Amesajiliwa kuziba nafasi ya Jean Charles Ahoua, ambaye ameuzwa kwenda CR Belouizdad ya Algeria.

Kiungo huyo anakuwa mchezaji wa tatu raia wa Senegal kuitumikia Simba, akifuata nyayo za Pape Ndaw na Pape Ousmane Sakho.

KISM 08

DJIBRILLA KASSALI

Ni usajili uliotokana na changamoto iliyoikumba Simba baada ya kumkosa kipa wao namba moja, Moussa Camara, ambaye aliumia akiwa na timu hiyo mwanzoni mwa msimu huu, pamoja na majeraha ya kipa namba mbili, Yakoub Suleiman.

Hali hiyo ilisababisha uongozi wa Simba kumtoa Camara kwenye mfumo wa usajili ili kupunguza idadi ya wachezaji wa kigeni, lakini pia kufuata kanuni inayoruhusu timu za ligi kusajili kipa mmoja wa kigeni.

Kassali ametokea AS FAN ya kwao Niger, timu ambayo imeshiriki michuano ya CAF mara tano; Ligi ya Mabingwa Afrika 2011, 2017 na 2018, huku Kombe la Shirikisho Afrika ikiwa ni 2009 na 2010, ilipofikia hatua ya robo fainali.

Tayari amejihakikishia nafasi ya kuingia moja kwa moja katika kikosi cha kwanza, licha ya uwepo wa Hussein Abel, ambaye ni kipa namba tatu kwenye kikosi hicho.

KISM 07

DEPU

Laurindo Wilson Maria Aurelio ‘Depu’ ni mshambulaji mpya wa Yanga ambaye tayari ameanza kuonyesha makali yake Ligi Kuu Bara, kwani katika mechi mbili amehusika kwenye mabao manne, akifunga matatu na kutoa pasi moja ya bao.

Depu amesajiliwa akitokea Ligi ya Poland, hatua inayodhihirisha dhamira ya mabingwa hao wa Ligi Kuu Bara kuongeza nguvu katika safu ya ushambuliaji kuelekea nusu ya pili ya msimu.

Mshambuliaji huyo raia wa Angola anakamilisha idadi ya wachezaji watano waliosajiliwa na Yanga katika dirisha hili dogo. Wengine ni Emmanuel Mwanengo, Mohammed Damaro, Allan Okello, Hussein Masalanga.