Hatimaye Iran wapewa viza kuingia Marekani
Muktasari:
- Uidhinishaji huo umekuja siku 10 tu kabla ya mechi ya kwanza ya Iran dhidi ya New Zealand, ambayo imepangwa kuchezwa mjini Los Angeles tarehe 15 Juni.
LOS ANGELES, MAREKANI: WACHEZAJI na viongozi wa Timu ya taifa ya Iran imepewa viza ya kuingia Marekani siku chache kabla ya kuanza kwa Kombe la Dunia wiki ijayo, maafisa wa Marekani wamethibitisha.
Uidhinishaji huo umekuja siku 10 tu kabla ya mechi ya kwanza ya Iran dhidi ya New Zealand, ambayo imepangwa kuchezwa mjini Los Angeles tarehe 15 Juni.
Maafisa wa Marekani walisema:”Viza muhimu kwa Iran kushiriki Kombe la Dunia, ikiwemo vya wachezaji na wafanyakazi muhimu wa timu, vimetolewa.”
Hata hivyo, waliongeza kuwa Marekani haitaruhusu timu ya Iran “kutumia mfumo huo vibaya kwa kuingiza magaidi nchini Marekani kwa visingizio vya uongo.”
Shirikisho la Soka la Iran bado halijatoa tamko rasmi kuhusu kupatikana viza hivyo.
Hii itakuwa mara ya kwanza katika historia ya mashindano hayo kwa nchi mwenyeji kupokea timu kutoka taifa ambalo iko katika hali ya vita nalo. Mwishoni mwa Mei, Iran ilihamisha kambi yake ya mazoezi kutoka Tucson kwenda Mexico. Rais wa Shirikisho la Soka la Iran, Mehdi Taj, alisema hatua hiyo ilitokana na matatizo ya viza.