Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

EXCLUSIVE: Sunday Manara, nilikataliwa Bongo, Ulaya ikanipa heshima

TANZANIA wamepita nyota wengi wa soka wenye uwezo mkubwa uliowapa umaarufu na kati ya wachezaji hao huwezi kuacha kuizungumzia familia ya Ramadhani Manara na mkewe Mishi Mikessy.

Mwenyezi Mungu aliijalia familia hii watoto saba, wakiwamo watatu wa kiume walioacha alama katika soka la Tanzania kwa umahiri wao wa kusakata kandanda.

Watoto hao ni Kitwana Manara ‘Popat’, Sunday Manara ‘Computer’ na Kassim Manara waliowahi kutamba na timu za Yanga, Pan Africans na Taifa Stars mbali na kucheza soka la kulipwa nje ya nchi.

Mwanaspoti limemtafuta mmoja ya wakongwe hao, Sunday Manara, baba mzazi wa supastaa, Haji Manara ‘Bugatti’ na kufanya mahojiano maalumu na mwamba huyo kufunguka mambo makubwa.

Gwiji huyo aliyeitumikia Yanga miaka ya 1970 kabla ya kwenda kucheza soka la kulipwa Uholanzi akiwa mchezaji wa kwanza wa Kitanzania kusakata soka barani Ulaya na kucheza michuano ya Klabu Bingwa ya Ulaya (sasa Ligi ya Mabingwa Ulaya). Ebu tiririka naye upate uhondo...!


UJIJI KIGOMA

Sunday anasema amezaliwa Kigoma Ujiji, baba yake alikuwa askari, hivyo maisha yao yalikuwa ya kuhamahama na kuwafanya watoto wa familia hiyo kuzaliwa sehemu tofauti.

Miongoni mwa watoto wa Mzee Manara, wapo waliozaliwa Kigoma, Dar es Salaam na Dodoma na kikubwa ni kwamba familia yao iliupenda sana mchezo wa mpira wa miguu, kaka yake Kitwana Manara aliitumikia Yanga kipindi hicho. Kitwana aliyecheza soka la kulipwa nchini Kenya katika timu ya Feisal FC, alicheza nafasi mbili tofauti kwa wakati mmoja, akiwa kipa na pia ni mshambuliaji. Akiwa Yanga alikuwa straika tishio na kuichezea timu ya taifa, alikuwa kipa hodari na kumfanya aweke rekodi ambayo haijavunjwa hadi leo akiwa amestaafu soka kitambo.


KUKATALIWA

Sunday anasema katika maisha yake akiwa anasoma shule hakuwahi kukubaliwa na wanafunzi wenzake kama mwanasoka, hivyo hakupata fursa ya kuwa hata mchezaji katika darasa alilokuwa akisoma.

“Kipindi hicho nilikuwa na mwili na umri mdogo, hivyo hakuna aliyekuwa anamfikiria kama nina uwezo wa kucheza soka.

“Sikuweza kuaminiwa hata na wanafunzi wenzangu kuitumikia timu ya darasa, kwani sikuonekana kama najua chochote katika mchezo huo.

“Ila baada ya kumaliza shule wakati huo wengi hawakuamini kama yule asiyejua lolote ndiye anayechezea timu ya taifa, ilikuwa ni ndoto iliyotimia,” anasema Sunday.


SAFARI YA SOKA

Sunday anasema alipenda soka, hivyo alijifunza kwa kasi ya ajabu hali iliyomfanya kujua vitu vingi ndani ya muda mfupi.

“Nilikuwa mtumwa wa mpira na niliwekeza muda na akili yangu kwenye mchezo huo, hivyo niliweza kuonekana na kukubalika na watu. Kama nakiona kitu kilichofanywa na mchezaji, ujue sio chake tena hicho, kimeshakuwa cha kwangu,” anasema na kuongeza;

“Ukiunganisha ujuzi wangu ilinifanya niwe mtu hatari kwa kipindi hicho hata mashabiki hawakuelewa ilikuwaje nikawa mkali, hapo wakaanza kunipenda ghafla.”

Sunday anasema alianza soka kama mchezaji wa mtaani katika timu ya Buguruni Stars, kisha akajiunga na Young Kinya na baadaye timu B ya Yanga iliyokuwa ikiitwa African Boys.


KUTUA YANGA

Anasema alianza kuitumikia Yanga ya wakubwa mwaka 1969 baada ya kipaji chake kuonekana na huko alicheza na kaka yake, Kitwana Manara na mdogo wake, Kassim Manara.

“Usajili wangu haukuwa wa fedha kama nilivyosema nilianza kucheza kama mchezaji niliyepanda kutoka timu B hivyo nilicheza kwa mapenzi na kupata huduma za kawaida tu.

Sunday anasema kaka yake Kitwana aliyekuwa nyota maarufu wa Yanga miaka ya 1960-1970 alirahisisha safari yake ya kutua Yanga, akianzia timu ya vijana wadogo ya Yanga B.

Anasema kaka yake kabla ya kwenda Yanga, alikuwa kipa wa Stars, pia alicheza Feisal ya Mombasa na TPC Moshi.

Nyota huyo anasema alipata bahati ya kupendwa sana na kupewa nafasi ya kucheza hadi timu ya taifa akiwa na umri wa miaka 17 tu.


MECHI YA KWANZA YA DERBY

Sunday anasema mechi yake ya kwanza dhidi ya Sunderland (Simba) (hakumbuki ilikuwa ni lini), aliingia kipindi cha pili na alipougusa tu mpira alipiga shuti ambalo lilikuwa bao.

“Mechi za Simba na Yanga huwa zinawapa watu umaarufu na ikitokea mchezaji wa timu yoyote akapata nafasi ya kufunga basi anakuwa maarufu sana.

“Mchezo huo tuliwafunga mabao 2-0 la kwanza lilifungwa na kaka yangu Kitwana na kumalizia la pili. Kuanzia hapo nikachaguliwa kwenda kucheza timu ya taifa na ile ya mkoa.

Anasema amekuwa na bahati ya kupata umaarufu akiwa kijana mdogo sana kabla hata hajapewa chumba cha kulala nyumbani wakati huo anajulikana kama mchezaji wa timu ya taifa akiwa bado analala varandani.

Anasema kijana mdogo hawezi kupewa chumba wakati huo ila anapewa nafasi varanda ndio kama chumba chake na hapo ataweka mkeka na kuhifadhi nguo zake kwenye mfuko na asubuhi kukikucha unakuwa wa kwanza kuamka kabla ya wengine.

“Nilichaguliwa kwenda kucheza na timu ya taifa katika michuano ya Chalenji jijini Nairobi na kocha alikataa kunichezesha kwani nilikuwa mdogo,”

“Ikafuatia mechi ya pili na Uganda na walikuwa na timu nzuri sana wakati huo na ndio walikuwa wanaongoza katika Afrika Mashariki.”

Anasema wakati huo alipewa nasaha nyingi sana kabla ya kuingia uwanjani kwani alikuwa mdogo, hivyo kocha alihofia ataumizwa.

“Mechi hiyo ilishangaza watu kwani nilipiga chenga hadi wachezaji hawakuelewa nini wafanye kwani sikukamatika uwanjani niliweka juhudi ili tu nisiumie,” anasema.

“Hali iliyopelekea mashabiki wa Nairobi kuingia uwanjani na kunibeba juu juu na nikapata umaarufu sana nchini Uganda.”


KOCHA ROHO JUU

Manara anasema baada ya kurudi Tanzania, kocha Profesa Victor Stansculescu kutoka Romania ndiye aliyekuwa akiinoa Yanga kipindi hicho alinifuata nyumbani.

Anasema, alisikia kelele nje watu wakimuita Mzungu Koko ikabidi afungue mlango na kukutana na kocha uso uso mlangoni.

“Akaniomba twende nyumbani kwake Kariakoo Fire, kula chakula cha jioni na alipofika akamwambia mkewe alete mkataba wake na kumuonyesha mshahara wake ambao ulikuwa ni Sh 2,600 kwa mwezi,”

“Kocha aliniambia mimi ni kijana mdogo na ananihitaji, hivyo hatakiwi kunipoteza kwani anaipenda kazi yake na ndio inayoendesha maisha yake.”


ADHABU YA AJABU

Sunday anasema baada ya usia na pongezi kutokana na kupata ushindi na umaarufu kocha huyo alimpa Sunday adhabu ya aina yake.

Anasema alipewa adhabu ya kutaka awe mtiifu na kuingia uwanjani ili azidi kuwa bora ili mshahara wake kama mwalimu uendele.

“Kuanzia leo utakuwa unanitii bila maswali na amri ya kwanza utarudi kwenu Buguruni kwa miguu. Kila siku utakuja uwanjani nusu saa kabla ya wenzio na utaondoka nusu saa baada ya wenzako na hutacheza kipindi cha kwanza japo una uwezo mkubwa.”


JINA LA KOMPYUTA

Jina hili lilikuja mwaka 1975 katika mchezo wa Yanga dhidi ya Simba katika michuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki (Kombe la Kagame) na pia kung’ara kwenye mechi za Klabu Bingwa Afrika (sasa Ligi ya Mabingwa Afrika).

Anasema kuwa katika mashindano hayo mtangazaji wa mchezo huo alikuwa akipenda sana mavitu yake na akamuita Kompyuta.

“Baada ya mchezo huo narudi nyumbani nakutana na jina hilo wakati huo hata hizo kompyuta tulikuwa hatuzifahamu ila mtangazaji huyo aliniita hivyo na watu wakaliendeleza.

“Nilishangaa kusikia naitwa kompyuta, sikujua kitu hicho ni kitu gani, ila ninachokumbuka nilisikia kwa mara ya kwanza mashabiki wakiniita kompyuta mwaka 1975.

“Jina hilo lilivuma na kuzoeleka, niliamua kuuliza maana ya kompyuta ni nini nikaambiwa ni mashine inayopiga hesabu kwa haraka sana,” anasema Manara.

Anasema licha ya kulikubali jina hilo, lakini hakuwahi kuiona hiyo mashine hadi alipokwenda Ulaya na kuishuhudia kwa macho miaka mitatu baadaye.


USHIRIKINA BALAA

Sunday anasema ushirikina upo kwa asilimia kubwa katika mpira wa miguu ila kwa enzi zao mambo yalikuwa ni ya kutisha kipindi hicho.

Anasema hata wakati anacheza alikumbana nayo matendo hayo kwenye timu alizocheza, japo huwa haamini vitu hivyo kwa kujua soka ni sayansi na mazoezi na sio imani hizo.

“Ningeweza kuandika kitabu kuhusu ushirikina kwani nimeuona lakini bado siuamini kwani tulitumika wachezaji bora katika michezo yote.

“Lazima nikubaliane na timu ili kuondoa mzozo na wenzangu kwani wangepata matokeo mabaya lawama zote zingehamia kwa yule aliyegoma kushirikiana na wenzake.”


HISTORIA YA DERBY

Sunday anasema kipindi hicho mechi za watani wa jadi zilikuwa na upinzani mkali sio sawa na sasa kwani enzi hizo walikutana mara moja kwa mwaka.

Anasema kuwa derby ya mwaka 1974 ilikuwa balaa, kwani msimu wa nyuma walitoka kufungwa baada ya kuiburuza Simba kwa misimu mitano mfululizo na maandalizi ya mechi hiyo iliyopigwa Uwanja wa Nyamagana Mwanza yalikuwa bab’kubwa.

“Maandalizi ya mechi hiyo ya 1974 yalikuwa makubwa kwa pande zote mbili hasa Yanga kwani walikuwa wanahitaji sana ushindi. Sisi tulienda Brazil kwa maandalizi tukatembea sana hadi tukapata ajali ya ndege tuliporudi tulikuwa Simba wamekuwa bora zaidi.

“Viongozi wa Yanga walikuwa na ari na hamu ya kupata ushindi hivyo wakatupeleka kuangalia World Cup (Kombe la Dunia) Ulaya ili tu tupate maarifa ya kuwafunga Simba.”

Anasema baada ya kurudi kutoka Ulaya tulifikia Nyegezi, jijini Mwanza tukaweka kambi na tulifanya mazoezi magumu na kwa siku mara tatu yaani asubuhi, jioni na usiku.

Sunday anasema walipokea bao la mapema kutoka kwa wapinzani wao, lakini mechi hiyo iliisha kwa 2-1, baada ya mchezaji huyo kufunga bao dakika za mwisho.


AKATAA OFA YA SIMBA

Sunday anasema Simba ilimhitaji na ikamtuma mchezaji wake Abdallah Seif ‘Kibadeni’, alipokwenda kuzungumza nao hakuwaelewa lakini alipokea pesa.

Anasema Simba hawakuwa wazi kwake, kama wanamhitaji japo hakukuwa na mikataba enzi hizo.

“Baada ya kupokea Sh. 3, 000 kiasi ambacho wakati huo kilikuwa na uwezo wa kununua nyumba tatu Kariakoo, uvumi ulikuwa mkubwa kuwa nimepokea pesa na nimehama Yanga.”

Anasema hakuweza kabisa kutoka Yanga kwa muda huo, kwani ilionekana kama laana hivi kwa sababu alikuwa mtoto wa pale.

“Uongozi wa Yanga uliniita na nilikiri kupokea pesa ndipo walipotangaza kwa Simba wakachukue pesa zao na wakanipatia Shilingi 50.”


SIRI YA KIBADENI

Sunday anasema yeye na Kibadeni ni marafiki hadi sasa kwani wakati wanacheza Simba na Yanga walikuwa wapo wote katika timu ya taifa hali iliyowakutanisha mara nyingi.

Manara anasema yeye na Kibadeni wamekulia sehemu moja mitaa ya Buguruni na Ilala hata walipoanza safari ya soka waliianza wakati mmoja.

“Simba walimtumia Kibadeni wakati huo kwa sababu alikuwa akiniweza sana, hivyo isingekuwa ngumu mimi kumgomea dili hilo. Hadi leo Kibadeni ni rafiki yangu hata kama akitaka kuozesha naweza kuwa Sheikh nitakayefungisha ndoa ya mwanaye hivyo tumekuwa ndugu sasa.”


YANGA KIMATAIFA

Sunday anasema wakati huo walicheza wazawa hakukuwa na mchezaji wa nje, hivyo walicheza kwa bidii sanaa kwani Yanga ilikuwa mali yao.

Anasema wakati huo hakukuwa na kutafuta maslahi ila ni mapenzi ya dhati na timu, walicheza mechi na Abaluya (AFC Leopards) bila kutaka pesa yoyote kwani walitaka kununua nyumba yao ili waweze kuepukana na kodi za pango.

Tulinunua nyumba Mtaa wa Nyamwezi kwa Sh 11,000 wakati huo nyumba hazikuwa na thamani kubwa kama sasa.

“Kabla ya Karume kuja kutuwezesha na matajiri wengine ambao waliifanya Yanga kumiliki mabasi na wao kuwa na nyumba za kuishi tulikuwa choka mbaya,”

“Bila kujali tunapata nini tuliitumikia na kufanya vizuri kimataifa kwani tulikuwa na uchungu na vipaji vyetu na timu yetu.”


UHUSIANO NA PLUIJM

Sunday anasema, Kocha Hans Pluijm alikwenda Uholanza na akaulizwa kuhusu yeye lakini kwa bahati mbaya hakuwa ananifahamu.

Anasema Pluijm aliwatafuta Yanga ndipo akapewa taarifa zangu na aliporudi tena kuitumikia Singida alimtafuta na wakaonana.

“Kocha Hans (Pluijm) hakujua kabisa kama kungekuwa na Mtanzania ambaye amafahamika nchini kwao licha ya kuwa na wachezaji wazuri.”