Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Edo Christopher: Mshkaji alinitambulisha kwa ex wangu

Muktasari:

  • Nyuma ya Kamera awamu hii imepiga stori na nyota huyo ambaye mwaka 2012 akiwa Simba B alinyakua kiatu cha ufungaji bora wa mabao manane katika michuano ya Super8 timu hiyo ikichukua ubingwa, kisha akapandishwa kikosi cha wakubwa.

JE, unamkumbuka mshambuliaji wa zamani wa Simba, Edward Christopher anayekipiga Stand United ya Shinyanga inayocheza Ligi ya Championship, nyota huyo amepitia mikasa mingi ya kimaisha inayoweza kukufunza jambo.

Nyuma ya Kamera awamu hii imepiga stori na nyota huyo ambaye mwaka 2012 akiwa Simba B alinyakua kiatu cha ufungaji bora wa mabao manane katika michuano ya Super8 timu hiyo ikichukua ubingwa, kisha akapandishwa kikosi cha wakubwa.

Miaka ya nyuma alikuwa miongoni mwa vipaji vikubwa vilivyokuwa vinatabiriwa kufika mbali katika soka, pamoja na hilo kama binadamu ana maisha ya kawaida ya kufurahisha na kuhuzunisha.

Kwa mara ya kwanza kitu ambacho wengi hawajawahi kukijua, anasimulia aliwahi kumpenda mrembo mmoja na ilifikia hatua akawa anajiamulia mambo bila kuzingatia tamaduni za Kitanzania.

Alianza kumpenda msichana huyo tangu akiwa anacheza Simba na licha ya umaarufu wake alikataliwa, hilo lilimfanya aendelee kuvutiwa kuona yupo tofauti na wanawake wengine ambao majibu yao ni kama walikuwa wanasubiri kuambiwa wanapendwa.

"Sikukata tamaa, ombi langu alilikubali wakati nacheza Toto Africans ya Mwanza, lakini akawa anaogopa historia ya mahusiano yake ya  nyuma, kutokana na kumpenda sana sikutaka hayo yawe kikwazo kwani hata mimi nilikuwa na ya kwangu, hivyo nilitaka tuwe na ukarasa wetu mpya pamoja," anasema na kuongeza;

"Nilikaa naye takribani  miaka miwili nikiwa tayari nimehamia Kagera Sugar, hivyo nikawa nimezoeana hadi na mama mkwe nikawa namkopa pesa, mfano kodi ikiisha namwambia mama mkwe nikopeshe nikipokea mshahara nakurudishia pesa yako na nilikuwa narudisha.

"Kuna siku nilimwambia kwa muda niliokaa na wewe nahitaji kwenda kupeleka posa nyumbani kwenu, akakubali nikamwita mshkaji wangu anisaidie kuandika barua inavyotakiwa, sikumbuki vizuri kama siyo Sh50,000 itakuwa ilikuwa Sh100,000 niliyokuwa nimeambatanisha na barua.

"Mapenzi yanitia upofu hadi nilikuwa sijajua natakiwa nikae chini na familia yangu ndiyo ipeleke barua, nilimtafuta mtu mtaani nilikokuwa naishi, jamaa mmoja  alikuwa kibonge ni bodaboda aliyekuwa ananibeba katika mizunguko yangu, kutokana na mwili wake nilijua watampa heshima ya mjomba.

"Baada ya yule boda kukubali nikaenda kumtafutia koti la heshima sikutaka avae la bodaboda, kisha tukaenda hadi ukweni ambako walitupokea vizuri na tukajibiwa mahari natakiwa kutoa Sh.2. 5 milioni, hiyo haikuwa shida kwangu kutokana na pesa ambayo nilikuwa napata Kagera."

Anasema hata hivyo penzi likaishia njiani na ameolewa na mtu mwingine na amezaliwashwa, hivyo wamebakia kuheshimiana kama dada na kaka.

"Nilijifunza mwanamume anayetaka kuoa asikurupuke, huwezi kumjua mwanamke kwa kipindi kifupi, pia wengi wao wanajikuta wanapata shida katika ndoa zao kutokana na maagano wanayoyaweka huku halafu wanakwenda kuolewa ama kuoa kule, hivyo ni vizuri mtu  anapoanza mahusiano mapya awe amefuta historia za viapo vingine," anasema na kuongeza;

"Baadaye nikaona nilikuwa na mambo ya ajabu, kwani nilianza kuona ndugu zangu wanapotaka kwenda kupeleka barua, inakaa familia, sasa mimi sikuwahi kumjulisha mtu yoyote wa familia zaidi ya kuona bebi amekubali, sikuwaza maisha mengine nje na momenti za mahaba na mapenzi mazito kabla hayajafa."

Ingawa kwa sasa anakiri ana mtu wake, lakini anajipa muda wa kuoa kwani anaamini maisha ni zaidi ya mapenzi, hivyo anahitaji mwenza wake awe ni yule atakayepambana naye katika vipindi vya furaha na huzini.

"Ukiachana na tukio hilo, kuna msichana aliniomba namba katika mitandao ya kijamii kipindi cha nyuma, tulianza urafiki kisha tukawa wapenzi, ingawa sikuwahi kulala naye, kuna siku mshikaji wangu alinipigia simu anamleta shemeji nimfahamu nikashangaa ni yule niliyekuwa nachati naye jumbe za kimapenzi kwenye simu na alikula pesa zangu kuna wakati nilikuwa nampa Sh. 5000, 10,000 wakati mwingine hadi 50,000, ukiacha hivyo nilimnunulia sana umeme hadi nikawa nafahamu namba ya Luku.

"Baada ya kuniona natambulishwa mimi na mpenzi wake, alishtuka sana, ila nikachukulia poa baada ya jamaa kutuachia mpenyo nikamwambia awe na amani, sitaki kuwasiliana naye tena na amheshimu jamaa, kwani mwanamume anapotoa pesa wakati mwingine anakuwa amejinyima, hivyo siyo jambo jema kula pesa ya mtu usiyempenda."

Pia anasema amekuwa akifunza vitu vingi kutoka kwa msaanii wa Bongo Fleva, Ben Pol aliwahi kumsikia akisimulia jambo: "Alisema watu wengi maarufu wanaposhuka kimaisha, inakuwa inawapa msongo wa mawazo, wanajikuta wanapoteza uelekeo wa ndoto zao.

Anaongeza: "Baada ya kuachana na Simba mtaani walikuwa wananinyooshea vidole kila mtu aliongea lake, nikajikuta nakutana na washkaji wananiambia kunywa bia mbili, tatu utakaa sawa na huo ndio ukawa mwanzo wa kunywa pombe, ila nilipokaa chini na kukubaliana na hali basi nikaachana na hayo, nikaweka nguvu katika kupambana."