Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Baada ya kichapo, Guardiola aibadilishia mbinu Real Madrid

TOLEO lililopita katika Pep Confidential, Mwandishi Marti Perarnau alizungumzia kipigo cha mabao 4-0 ambacho Bayern ilikipata nyumbani kutoka kwa Real Madrid pamoja na tukio la hotelini ambako Bayern walipatumia kwa mlo wa jioni na kujadili mechi. Sasa endelea...

Eneo lenyewe ni chumba kimoja kwenye Hoteli ya Intercontinental mjini Madrid ambako Bayern walipatumia kufurahia mlo wa jioni kama ilivyo utamaduni wao wa siku zote na huko kidogo wanapata wasaa wa kujadili mechi yao ilivyokuwa.

Watu wote walikuwa wameshapata chakula lakini meza tatu zilikuwa tupu, chakula cha jioni kilichobaki kilihusisha watu wa habari, kundi la wafadhili wa Bayern na meza ya tatu ni kwa ajili ya Pep na wasaidizi wake katika benchi la ufundi.

Tayari kundi lile lilikuwa limeshachambua kini cha tatizo lao hadi kufungwa bao 1-0 mjini Madrid kwenye Uwanja wa Bernabeu na walijivunia namna ambavyo wachezaji wao walishikamana na mpango mzima wa mechi yao.

Pia, walifahamu ukweli wachezaji wao walikuwa chini ya kiwango na walikuwa wakihaha kuikabili safu ya ulinzi ambayo ilikuwa imejipanga vizuri, yenye wachezaji wenye vipaji vya hali ya juu ambao wanakaba wakiwa katika ubora.

Pep hadi hapo tayari alikuwa mwenye kutatizwa katika maisha yake ya ukocha wa soka; unawezaje kushambulia kwa ubora katika mazingira magumu kama hayo?

Mara kwa mara suluhisho la mazingira kama hayo ni kushambulia kwa kufumua mashuti ya nguvu golini, Bayern ilipiga mashuti kwenye lango la Real Madrid mara 18 kwenye Uwanja wa Barnabeu karibu mara mbili zaidi ya wapinzani wao.

Jambo la pili lilikuwa ni kupiga krosi ambazo zingeenda moja kwa moja katika eneo la boksi na kumkuta mshambuliaji. Bayern ilipga krosi za aina hiyo mara 31 ambayo ni kama mara tatu zaidi ya wapinzani wao.

Ukweli katika soka unapoamua kutumia mfumo wa Pep wa kukama maeneo dhidi ya timu ambayo inakaba vizuri mwanzo mwisho, kunahitaji si tu maandalizi ya kiwango cha juu, bali pia ubunifu wa mchezaji binafsi.

Kwa maneno mengine katika mazingira ya aina hii magumu na ya kuchanganya hapo linakuwa ni jukumu la mchezaji mwenye kipaji na kiwango cha juu kufanya mambo yake.

Ni bahati mbaya sana wakati wa mechi, washambuliaji wote wa Bayern ni Arjen tu ndiye aliyekuwa katika ubora wake, wengine ni ama walishindwa kuwapenya wapinzani wao au walishindwa kupiga mashuti sahihi kwa sababu walibanwa na mabeki wa timu pinzani.

Ni saa tisa inaelekea saa 10 alfajiri ya Aprili 24, Pep alikuwa katika tafakari, alijiaminisha Madrid wangekuwa wa kufumua mashuti katika mechi ya marudiano kwenye Uwanja wa Allianz Arena, na hivyo alikuwa akijipanga kwa kutumia silaha zilezile na mipango ileile kama ilivyokuwa katika mechi ya kwanza.

Hapo alimjuisha Robben ambaye alikuwa katika kiwango cha juu, Ribery ambaye alikuwa na mambo mengi yaliyoharibu kiwango chake, Mandzukic ambaye aliishia kuuwahi mpira mmoja tu wa kona kati ya 15 zilizopigwa na timu yake kwenye Uwanja wa Bernabeu pamoja na Muller aliyekuwa mpambanaji.

Pep pia katika akili yake alikuwa akisumbuliwa na maneno ya Garry Kasparov, yule mkali wa mchezo wa chess duniani, “Pep kumbuka huwezi kushinda mchezo kwa sababu tu umesogeza kete zako mbele.”

Ni katika tafakuri hiyo ya alfajiri ndipo Pep alipoamua katika mechi ya marudiano angetumia mfumo wa 3-4-3, akiwa na mabeki watatu wa katikati, mabeki wa pembeni wawili waliosogezwa mbele eneo la kiungo, karibu na viungo wabunifu pamoja na Gotze akiwa mmoja wa washambuliaji wawili ili awe na nguvu eneo la kati ya uwanja kwa washambuliaji hao kushuka na kutoa msaada.

Kwa hiyo ni mfumo wa 3-4-3 ambao angeweza kuubadili wakati wowote na kuwa ule wa kawaida wa 3-5-2 ambao unaruhusu kufanyiwa mabadiliko madogo.

Kimsingi alijiweka katika mazingira mazuri ya kukaba yanapotokea mashambulizi ya kushitukiza.

Pep alijiaminisha mashambulizi ya aina hiyo yangekuwa mengi mno, lakini pia mfumo huo ungewaruhusu Bayern kutawala eneo la kati ya uwanja, kutulia na mpira na kutobanwa pale inapotokea wamejazana eneo la penalti la Madrid.

Na hapo ndipo Pep aliposikika akimwambia, Torrent: “Nimemaliza, usiwe sababu ya kunifanya nibadili mawazo yangu, hii ndio njia ya kuikabili Real Madrid.

Itaendelea Jumamosi ijayo…