Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Dili iliyokufa - 12

HADITHI Pict

ILIPOISHIA

Alfajiri ya siku ya pili yake Sharifa aliamka akatoka uani akiwa na simu yake mkononi. Akampigia mwanawe Majaliwa.

Simu iliita sana kabla ya kupokelewa. Ilipopokelewa sauti ya Majaliwa ilikuwa nzito ikionesha  kuwa aliamshwa usingizini.

“Shikamoo mama”

“Marahaba. Yaani bado umelala hadi muda huu?”

“Niliamka mapema”.

SASA ENDELEA...


“Muongo wewe, sauti yako inaonesha kuwa unatoka usingizini halafu unasema uongo wako”

Mjaliwa akanyamaza kimya.

“Unakumbuka jana tulizungumza nini?”

“Nakumbuka”

“Kama unakumbuka mbona dado umelala wakati nilikwambia upige simu saa moja asubuhi”

“Saa moja bado mama”

“Sasa kama nisingekuamsha ungeamka saa ngapi?”

“Mmmh! Mama unapenda kesi sana. Sasa mimi nimeshaamka. Ikifika saa moja nitapiga simu”

“Lakini unakumbuka vile nilivyokufundisha?”

“Nakumbuka”

“Usije ukazungumza vitu vinginevyo”

“Hapana. Nakumbuka kila kitu”

“Sawa. Sasa wewe subiri ukiona imefika saa moja piga simu, akipokea utajieleza na mimi nitakuwepo”

“Sawa”

Sharifa akakata simu na kurudi chumbani. Wakwetu naye alikuwa ameshaamka akashuka kitandani na  kuingia maliwatoni.

Saa iliyokuwa ukutani juu ya mlango iligonga kuonesha kuwa ilikuwa saa kumi na mbili kamili.

“Bado saa moja Majaliwa atapiga simu” Sharifa aliwaza kimoyomoyo. Kutokana na moyo wake kupata wasiwasi alitoka mle chumbani na kwenda kukaa sebuleni.

Alikuwa na wasiwasi kwamba endapo Majaliwa atakosea kujieleza, Wakwetu atampuuza na mpango wao utakuwa umekufa.

“Lakini namuamini Majaliwa. Najua hawezi kuzungumza upuuzi” akajiambia kimoyomoyo kujifariji.

Ili mume wake asitoke na kumuona amekaa hapo, aliinuka tena na kuingia jikoni. Aliwasha jiko akachemsha maji ya chai.

Saa ya ukutani iliyokuwa juu ya mlango wa jiko ikagonga kuashiria kuwa saa kumi na mbili na nusu.

Huko chumbani Wakwetu alioga na kuvaa. Mpaka inafika saa moja kasoro robo alitoka na kukaa sebuleni.

Alifungua tv na kutazama habari fupi zilizokuwemo kwenye magazeti ya siku ile. Alikuwa akisubiri saa moja kamili ili atazame taarifa ya habari.

Sharifa baada ya kuivisha chai aliitia kwenye chupa na kutoka. Alikwenda sebuleni alipoketi mume wake na yeye akaketi. Aliitupia macho saa ya ukutani iliyokuwa hapo sebuleni na kuona zilikuwa zimebaki dakika chache kabla ya kutimia saa moja kamili asubuhi.

“Umeamkaje?” akamuuliza hali mume wake.

“Nashukuru, nimeamka vizuri. Sijui wewe?”

“Mimi pia pia nashukuru, nimeamka vizuri”

Mara simu ya Wakwetu aliyokuwa ameishika mkononi ikaita. Sharifa akashituka na kumtupia macho.

Wakwetu alitazama namba iliyokuwa inaita kisha akaipokea simu na kuiweka sikioni, akasema.

“Hello!”

Kwa vile Sharifa alikuwa amekaa naye karibu aliweza kuisikia sauti ya Majaliwa ikisema.

“Shikamoo”

“Marahaba. Hujambo?”

“Sijambo. Nazungumza na mzee Wakwetu?”

“Ndiyo mimi, wewe nani?”

“Mimi mwanao, niko Nguvumali.”

“Mwanangu nani?”

“Hunitambui, nimekupigia hii simu baada ya kuona tangazo kwenye gazeti la jana…”

Wakwetu akamtupia macho Sharifa kisha akauliza.

“Kwa hiyo unataka nini?”

“Katika hilo tangazo ulikuwa unawatafuta watoto wako na mimi ni mmoja wa hao watoto wako”

“Una ushahidi wowote wa kuniimanisha kuwa wewe ni mwanangu”

“Yale maelezo uliyotoa yameonesha kuwa wewe ni baba yetu ambaye tuliambiwa kuwa ulikwenda Afrika Kusini wakati mama yetu akiwa na ujauzito wetu sisi. Mpaka tunazaliwa sisi tulikuwa hatukujui”

“Mama yako yuko wapi?”

“Tuliambiwa kuwa mama yetu alifariki baada ya kutuzaa sisi” Majaliwa alikuwa kama amesahau kidogo lakini hapo hapo akakumbuka. “Tuliambiwa kuwa mama alituzaa kwa operesheni lakini akafariki”

Wakwetu alimtupia jicho tena Sharifa kabla ya kuuliza kwenye simu.

“Mama yenu alikuwa anaitwa nani?”

“Alikuwa anaitwa Zainab.”

Wakwetu akashituka. Aliona maelezo ya kijana huyo yalikuwa na muelekeo.

Akamtazama tena Sharifa. Sasa uso wake ukiwa makini.

“Umesema wewe uko wapi?”

“Niko Kwaminchi.”

“Sasa ningependa nikuone ili nithibitishe maelezo yako”

“Niambie nije wapi?”

“Njoo nyumbani kwangu?”

“Ni wapi?” Majaliwa alijidai kuuliza lakini nyumba ya Wakwetu alikuwa akiijua ilipo.

Wakwetu akamuelekeza.

“Panda bodaboda nitakuja kukulipia”

“Asante baba, ninakuja sasa hivi”

Simu ikakatwa. Kidogo moyo wa Sharifa ulianza kwenda mbio. Hakuwa na uhakika kama mpango wao utafanikiwa.

“Kijana mwingine amejitokeza” Wakwetu alimwambia Sharifa baada ya kuiondoa simu sikioni.

“Umeonaje maelezo yake?” Sharifa alikimbilia kumuuliza ili kupata undani wa Wakwetu.

“Huyu ana maelezo yanayolingana kidogo, ndiyo maana nimemuita”

“Yanalinganaje”

“Amenieleza historia yake kwa ufupi, inaelekea anaweza kuwa mwanangu”

Sharifa akapata faraja moyoni.

“Atakuja na mwenzake?” akajidai kuuliza.

“Amesema mwenzake alikufa huko Zambia walikokuwa”

“Masikini!”

“Ameniambia waliamua kwenda Zambia baada ya yule mama wa kiarabu kuwaacha”

“Alikwambia amerudi lini kutoka huko Zambia?”

“Ameniambia alirudi hivi karibuni, hivi sasa anaishi Kwaminchi”

“Sasa unaona ushauri wangu umezaa matunda. Nilikwambia usishangae kwamba hao watoto wako hapa hapa Tanga. Wakiona hilo tangazo watajitokeza”

“Sasa ngoja tumsubiri, tumhoji vizuri”

“Lakini kwa upande wangu ninaamini kabisa kuwa  huyo ni mwananao kutokana na maelezo yake”

“Maelezo yake yanalingana”

“Huyo akija unamhamishia nyumbani kwako tu”

“Ni kweli”

Haukupita hata muda wa saa moja, simu ya Wakwetu ikaita. Wakwetu alipoitazama sikrini alimwambia Sharifa.

“Huyo anapiga tena”

Wakawetu  aliipokea ile simu.

“Hello!”

“Baba nimeshafika, niko nje” Sauti ya Majaliwa ikasikika kwenye simu.

“Umeitambua nyumba?”

“Nafikiri ndiyo hapa nilipokuja”

“Ngoja nitoke nikuone”

Wakwetu aliondoa simu sikioni akamwambia Sharifa.

“Ameshafika, ngoja nikamkaribishe ndani”

Wakwetu aliinuka akatoka nje ya nyumba yake. Alimkuta Majaliwa akiwa na kijana wa bodaboda mbele ya geti.

“Ndiyo wewe?” Wakwetu akamuuliza.

“Ndiyo mimi” Majaliwa akamjibu kwa uchangamfu.

“Bodaboda anadai kiasi gani?”

“Tulikubaliana atanileta kwa shilingi elfu tano.”

Wakwetu aliufikiria umbali wa kutoka Kwaminchi hadi pale, akatia mkono kwenye koti lake na kutoa shilingi elfu tano akampa yule kijana. Bodaboda ikaondoka.

“Karibu ndani” Wakwetu alimwambia Majaliwa huku akimtazama tazama. Alimtazama kuanzia usoni hadi miguuni.

Wakwetu na mjaliwa waliingia ndani. Wakiwa sebuleni Wakwtu alimwambia kijana huyo.

“Karibu ukae”

Kwanza majaliwa alimwamkia Sharifa akijifanya kama hamjui, kisha akakaa.

Sharifa akamtazama, na yeye akiigiza kama hamjui.

“Habari za huko?” akamuuliza.

“Huko ni kwema, sijui nyinyi hapa”

“Sisi hatujambo. Wewe ndiye uliyepiga simu baada ya kuona tangazo kwenye gazeti?” Sharifa akajipa kazi ya kuuliza maswali.

“Ndiyo mimi, nilikuwa namtafuta baba yangu kwa miaka mingi. Sasa nilipoona lile tangazo na lile jina la baba nilikuwa nalijua ndipo nikampigia kujitambulisha”

“Baba mwenyewe umemuona?”

“Nimemuona”

“Mimi ndiye mke wake. Kwa hiyo endelea kujitambulisha kwake ili aweze kukutambua vizuri”

Majaliwa akamtazama Wakwetu akijifanya mwenye nidhamu ya hali ya juu.

“Sasa baba kama nilivyokueleza kwenye simu mimi ni mwanao. Mimi ni mtoto wa Zainab. Nilizaliwa Magomeni na mwenzangu ambaye alifariki dunia tulipokuwa Zambia. Sisi tulijikuta tukilelewa na mama mmoja wa kiarabu ambaye alitueleza kwamba mama yetu alituzaa kwa operesheni na alikufa baada ya operesheni ile”

“Pole sana” Sharifa akajidai kpokufa tukachukuliwa na huyo mwanamke wa kiarabu akatulea”

“Aliwalea mpaka mlifikia umri gani?”

“Tulishamaliza kidato cha tatu alipotuacha na kurudi Oman”

“Aliwaacha kwa sababu gani?”

“Mume wake alifariki, akaona asingeweza kuishi peke yake akarudi kwao”

“Sasa ilikuwaje mkaenda Zambia?” Sharifa aliendelea kumuuliza maswali rahisi ili asibanwe na Wakwetu kwa maswali.