Wimbo wa Awilo, Harmonize kuachiwa Ijumaa hii

Wednesday April 21 2021
awilo pic
By Nasra Abdallah

Msanii wa muziki wa Bongofleva, Harmonize ameweka wazi jina la wimbo walioimba na Mwanamuziki kutoka Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo, Awilo Longomba kuwa ni ‘Attitude’ na kutaja siku utakaoachiwa.
Harmonize amefanya hivyo leo Jumatano Aprili 21, 2021 kupitia ukurasa wake kwenye mtandao wa Instagram ukionyesha cover la wimbo huo na wasanii aliowashirikisha.
Mbali na Longomba pia katika wimbo huo yupo  msanii wa siku nyingi anayeimba muziki wa Bolingo, H.Baba.
Aidha ameeleza siku ya kuuachia wimbo huo kuwa itakuwa Ijumaa hii ya Aprili 23, 2021.
Harmonize ametumia nafasi ya Awilo kuwepo nchini akiwa anarekodi filamu ya ‘A life to Regret' kufanya shughuli hiyo.
Mbali na Harmonize, Awilo alieleza kuna wasanii wengine ambao ataingia nao studio ambao hakuwa wazi kuwataja.

Advertisement