Wema Sepetu alijitabiria mtoto wa kiume
Muktasari:
- Katika mahojiano na vyombo vya habari mwaka 2019, Wema alieleza licha ya kupita kwenye changamoto za kiafya zilizokuwa zikimzuia kupata ujauzito kwa muda, bado alikuwa na matumaini makubwa ya kupata mtoto na alitamani sana mtoto wake wa kwanza awe wa kiume kwa sababu ya mtazamo wake wa kifamilia na ndoto ya kuwa na mrithi wa kiume nyumbani.
Katika kipindi kirefu cha maisha yake ya mapenzi na changamoto za uzazi, Wema Sepetu aliwahi kufunguka wazi kuhusu ndoto yake ya kuwa mama, akieleza mapema anatamani sana kupata mtoto wa kiume kama mzaliwa wake wa kwanza.
Katika mahojiano na vyombo vya habari mwaka 2019, Wema alieleza licha ya kupita kwenye changamoto za kiafya zilizokuwa zikimzuia kupata ujauzito kwa muda, bado alikuwa na matumaini makubwa ya kupata mtoto na alitamani sana mtoto wake wa kwanza awe wa kiume kwa sababu ya mtazamo wake wa kifamilia na ndoto ya kuwa na mrithi wa kiume nyumbani.
“I would love to have a baby boy first.” aliwahi kusema Wema katika mahojiano na vyombo vya habari.
Wema alieleza amekuwa akipitia safari ngumu ya kiafya na kihisia katika kutafuta ujauzito, lakini bado moyo wake haukukatishwa tamaa, akisisitiza furaha yake itakamilika siku atakapofanikiwa kupata mtoto wake mwenyewe.
“Napenda mtoto wangu wa kwanza awe wa kiume. Wa kwanza akiwa wa kiume ataweza kuwaongoza wenzake watakaofuata,” alisema Wema Sepetu.
Kauli hiyo ya “kutamani mtoto wa kiume” imekuwa kama aina ya kujitabiria au ndoto ya mapema aliyokuwa nayo kuhusu maisha yake ya uzazi, hasa kutokana na jinsi alivyokuwa akiizungumza kwa msisitizo mkubwa katika mahojiano yake.
Licha ya kila changamoto, Wema aliendelea kusisitiza upendo wake kwa watoto na matumaini ya siku moja kuitwa mama, jambo lililowagusa mashabiki wengi waliokuwa wakifuatilia safari yake ya maisha kwa ukaribu.