Wasafi waja na Tumewasha Tour

Wasafi waja na Tumewasha Tour

KAMPUNI ya Wasafi Media imetangaza kufunga mwaka na tamasha la 'Wasafi Tumewasha Tigo'.

Mkurugenzi wa kampuni hiyo, Naseeb Abdul maarufu Diamond, amesema tamasha hilo linatarajiwa kurindima katika mikoa saba.

Diamond aliiitaja mikoa hiyo kuwa ni Shinyanga, Mbeya, Arusha, Dodoma, Mwanza, Zanzibar, Dar es Salaam na Kahama ndio watajaofungua dimba.

"Mwaka unaelekea kuisha na kama wasafi hawaachagi mwaka uishe hivi hivi lazima waufunge kwa kishindo, hivyo tumekuja na tamasha la 'Tunawasha'.

Mbali na wasanii wa ndani, Diamond amesema kutakuwepo na wasanii wa nje ambapo wataanza kuwasili kuanzia kesho.

Mkurugenzi wa vipindi wa wasafi, Nelson Kissanga amesema tamasha hilo ni sehemu ya kurudisha shukurani kwa Watanzania kutokana na namna walivyowapokea.

Naye Mkuu wa vipindi wa Wasafi TV, Jamal Mustafa, amesema tamasha pamoja na mambo mengine, litatumika kuibua vipaji, kutoa zawadi mbalimbali ikiwemo gari aina ya Alteza, pikipiki na fedha taslimu.

____________________________________________________________

 By NASRA ABDALLAH