Vyuma vitano vinavyochipukia Bollywood
MUMBAI, INDIA. UKIZUNGUMZIA waigizaji warembo wa kike waliotamba kwenye Bollywood kwa zaidi ya miaka 20, bila shaka majina kama Priyanka Chopra, Aishwarya Rai Bachchan, Kareena Kapoor, Katrina Kaif, Madhuri Dixit, Kajol, Siridev, Karisma Kapoor, Preity Zinta na Shilpa Shetty Hayawezi Kukosekana kwenye orodha.
Lakini muda huu soko limebadilika na waigizaji wengi wa zamani wameanza kuondoka kwenye soko na sura mpya zinaonekana kwenye soko. Hawa hapa mastaa watano wakike wanaofanya vizuri kwenye soko hilo.
Kiari Advani
Muigizaji mrembo, Kiari Advani, 28, ameonyesha yeye sio tu kabarikiwa urembo bali pia kipaji cha kuigiza baada ya kuigiza kwa mafanikio katika filamu za Kabir Singh na Good Newwz. Filamu yake ya kwanza ni Fugly ya mwaka 2014. Kwa ramani anayoendelea kuichora kwenye Bollywood haitashangaza siku moja akivaa viatu vya akina Kajol. Hata linapokuja suala la sura na urembo kwa Kiari wala haboi.
Pooja Hedge
Ndoto za Pooja kuigiza na ‘Handsome’ wa India, Hrithik Roshan aliyetamba na filamu kama Kirrish, Koi Mil Gaya, War na Dhoom 2 zilitimia baada ya kuigiza pamoja kwenye filamu ya Mohenjo Daro. Pooja, 30, ni Muigizaji pisi kali anayechipukia kwenye Bollywood ambapo linapokuja suala la sura na muonekano lazima utoe pointi za kueleweka ukizingatia amewahi kuwa mshindi wa pili kwenye mashindano ya Miss Universe India mwaka 2010.
Disha Patani
Hauhitaji kushawishiwa sana kuhusu sura na muonekano wake. Filamu yake ya kwanza iitwayo Loafer ya mwaka 2015 ilifungua njia kwenye maisha yake ya uigizaji . Disha, 27, ameigiza kwenye filamu ya Kichina iliyofanya vizuri kwenye mauzo barani Asia ya Kung Fu Yoga ya mwaka 2017 ambayo ‘Steringi’alikuwa ni Jackie Chan.
Sara Ali Khan
Ni sura mpya kwenye Bollywood iliyowasapraizi watu kwa umbo na muonekano katika filamu ya Kedarnath iliyotoka mwaka 2018. Hii ndio ilikuwa filamu yake ya kwanza kuigiza. Baada ya hapo alionekana kwenye kama Simmba, Love Aaj Kal na Coolie No. 1
Sara hawaangushi mashabiki wake linapokuja suala la urembo na huvutia Zaidi akiwa katika mitupio ya kichokozi.
Urvashi Rautela
Hadi sasa ameshaigiza na wacheza filamu maarufu duniani kama Sunny Deol, Anil Kapoor na John Abraham. Urvashi, 26, mbali na kuwa muigizaji pia ni mwanamitindo.
Ni mshindi wa Miss Diva Universe India mwaka 2015 na mwaka huo huo akaiwakilisha India katika mashindano ya Miss Universe.
Filamu yake ya kwanza kuigiza Bollywood ni Singh Saab the Great (2013), baadaye akaonekana kupitia Sanam Re (2016), Great Grand Masti (2016), Hate Story 4 (2018) na Pagalpanti (2019).