Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Spidoch Band yaachia kichupa kipya fasta

Kiongozi wa Spidoch Band, Budas King

Muktasari:

Mwimbaji nyota wa muziki wa dansi anayeiongoza Bogoss Musica, Nyoshi El Saadat 'Sauti ya Simba' ni kati ya watakanogesha  onyesho la uzinduzi wa bendi mpya ya Spidoch iliyo chini ya Budas King.

SIKU chache kabla ya bendi ya Spidoch 'Wazungu Weusi' haijazinduliwa rasmi katika onyesho lililopangwa kufanyika Oktoba 27, kundi hilo limeachia kichupa kipya cha wimbo uitwao 'Wasamehe'

Video ya ngoma hiyo ni kati ya nyimbo 12 zilizopo kwenye albamu mpya iitwayo Michimbaki ambayo itatambulishwa kwenye uzinduzi huo wa bendi hiyo utakaofanyika Ukumbi wa Break Point, jijini Dar es Salaam.

Bendi hiyo ipo chini ya mwimbaji mkali wa muziki wa dansi, Budas King imeachia kichupa hicho leo Jumapili ikiwa ni utangulizi wa kutaka kuwaweka sawa mashabiki wa miondoko hiyo kabla ya uzinduzi rasmi.

Mratibu wa onyesho hilo litakalosindikizwa na burudani kutoka kwa Nyoshi El Sadaat na bendi nzima ya Bogoss Musica, Rhobi Chacha alisema maandalizi kwa ujumla yanaendelea na anaamini video hiyo mpya ya Wasamehe itaonyesha ni jinsi gani Spidoch Band wamepania kuleta mapinduzi kwenye muziki.

"Kila kitu kipo sawa hadi sasa, lakini nimefurahi kuona tayari Spidoch imeachia video ya moja ya nyimbo za albamu itakayoenda kuzinduliwa sambamba na kundi zima siku ya Oktoba 27," alisema Rhobi ambaye ni mwandishi wa zamani wa burudani wa Mwanaspoti na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Chama cha Muziki wa Dansi nchini (Chamudata).

Bendi ya Spidoch iliwahi kutambulishwa kwa mara ya kwanza mwaka 2017 kisha ikapotea hadi sasa inaporejea ikija kivingine na Nyoshi El Saadat alikakariwa juzi anafurahia ujio huo kwani utaongeza ushindani kwenye miondoko hiyo.