Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Siri ya Wema, Whozu hii hapa

Whozu Pict
Whozu Pict

Muktasari:

  • Wema amepiga stori na Mwanaspoti na kudai alikuwa anapenda sana mambo ya drama za mitandaoni kuhusu mpenzi anayekuwa naye lakini tangu amegundua ndio moja ya sababu ya kutodumu nao, penzi lake na whozu hafanyi hivyo.

SUPASTAA wa kike nchini, Wema Sepetu ameweka wazi tangu ameacha drama za mitandaoni ameona amedumu katika mapenzi na hiyo ndiyo siri kubwa ya kuendelea kuwepo na kipenzi chake Whozu.

Wema amepiga stori na Mwanaspoti na kudai alikuwa anapenda sana mambo ya drama za mitandaoni kuhusu mpenzi anayekuwa naye lakini tangu amegundua ndio moja ya sababu ya kutodumu nao, penzi lake na whozu hafanyi hivyo.

Alisema hadi sasa ana miaka mitatu na Whozu katika mapenzi kitu ambacho hapo nyuma alikuwa akipata mpenzi kufika nae mwaka inakuwa ni shughuli nzito.

“Siri ambayo wengi hawaijui ndiyo nawapa leo sasa na najua wengi wanajiuliza, nimewezaje kuwa na Whozu hadi leo hii, nimeachana na maisha ya drama za mitandaoni kuhusu mapenzi,” alisema Wema na kuongeza;

“Kwa muda mrefu nimekuwa sina raha. Nimekuwana huzuni, nimekuwa nikilia lakini pale ninapoanzisha mahusiano halafu hayadumu kwa muda mrefu, sasa tangu nilipokutana na Chibaba wangu (Whozu) nimeamua kubadilisha mfumo wa mapenzi na ndiyo maana  nimekuwa na raha na kudumu nae hadi leo.”

Wema na Whozu penzi lao walianza kama utani, kwani walikuwa marafiki wa kawaida na baadae wakawa  wakijificha chini ya ‘urafiki’ huo hadi hatimaye kufikia kufichua mahusiano huo mwaka 2022 baada ya Whozu kuachana na Tunda aliyekuwa mzazi mwenzie.