Shilole ajishtukia, akimbilia gym kunusuru penzi

Muktasari:
- Shilole aliyeanzia kwenye filamu kisha kugeukia muziki akitamba na ngoma kadhaa, kwa sasa amejikita zaidi katika shughuli za kuuza vyakula na amekuwa na muonekano wa tofauti na alivyokuwa miaka ya nyuma, jambo ambalo limemfanya ajishtukie mwenyewe.
MSANII nyota wa filamu na muziki anayejishughulisha pia na ujasiriamali, Shilole amejishtukia na fasta ameamua kukimbilia gym kupiga tizi ili kupunguza unene alionao kwa nia ya kuokoa penzi lake na jamaa aitwaye Rich.
Akizungumza na Mwananspoti, Shilole alisema ameanza mazoezi ya nguvu kila asubuhi na jioni ili kupunguza mwili aendane na mpenzi aliyenaye, kwani mwili alionao kwa sasa ni mkubwa kuliko wa mwenzie.
“Daah, nimeona nitapoteza penzi langu bure, nimekuwa mnene kumpita mpenzi wangu, kitu ambacho siyo sawa, hadi naonekana nipo na king'asti wakati ni mtoto mwenzangu," alisema Shilole na kuongeza;
"Mbali na kunusuru penzi langu, pia kunusuru afya yangu kwa kuepusha maradhi ya mara kwa mara, sema shida inakuja tu pale napenda kula, napenda kupungua pia, mbona kazi ninayo hapa, ila naimani nitashinda hii vita ya kupunguza unene."
Shilole aliyeanzia kwenye filamu kisha kugeukia muziki akitamba na ngoma kadhaa, kwa sasa amejikita zaidi katika shughuli za kuuza vyakula na amekuwa na muonekano wa tofauti na alivyokuwa miaka ya nyuma, jambo ambalo limemfanya ajishtukie mwenyewe.