Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Redds Miss Tabata kupatikana leo

Mwandishi Wetu MALKIA la Redds Miss Tabata 2012 atapatikana leo wakati warembo 19 watakapopanda jukwaani kwenye ukumbi wa Da’ West Park, Tabata. Mratibu wa shindano hilo alisema jana kuwa zitawasindikiza warembo 19 watakaopanda jukwaani kuwania taji hilo. Mratibu wa shindano hilo lililoandaliwa na Bob Entertainment na Keen Arts, Joseph Kapinga shindano hilo litapambwa na bendi za Mashauzi Classic na Mashujaa. Alisema mshindi wa kwanza kwenye kinyang'anyiro hicho atazawadiwa Sh 500,000/- na king’amuzi cha Multichoice kilicholipiwa miezi sita kwa thamani ya sh 800,000. Mshindi wa pili atapata sh 500,000, mshindi wa tatu sh 350,000 wakati washindi wa nne na watano kila moja atapata sh 200,000. Kapinga alisema warembo watano watawakilisha Tabata kwenye shindano la Miss Ilala. Warembo wengine watakaoingia 10 bora kila moja atapata sh 100,000 wakati waliyosalia watapata Sh 50,000 kila moja. Kapinga alisema shindano hilo pia litatumika kwa ajili ya kusherehekea miaka 10 tangu kuasisiwa kwa shindano la Redds Miss Tabata. “Shindano la mwaka huu sio la kukosa kwani litakuwa ni la aina yake ukizingatia kuwa litatumika kusherekea miaka 10 tangu kuanza kuandaa Miss Tabata,” alisema Kapinga. Warembo wa Tabata wamekuwa wakifanya vizuri katika mashindano ya Miss Tanzania ambapo mwaka juzi Consolata Lukosi alishinda nafasi ya tatu kabla ya kutangazwa kuwa balozi wa kinywaji cha Redds. Shindano hili limedhaminiwa na Dodoma Wine, Redds, Integrated Communications, Fredito Entertainment, Multichoice Tanzania, Screen Masters, Kitwe General Traders, Step In Electronics, Brake Point, Atriums Hotel na Lady Pepeta.