Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Paula afichua sababu ya kuanika uso wa mtoto mapema

Muktasari:

  • Akizungumza na Mwanaspoti, Paula aluiyejifungua Juni 3 amesema, sababu ya kwanza anajiamini na baba wa mtoto huyo, pia  kutaka pongezi ziweze kumiminika kwa wakati muafaka.

PAULA, binti pekee wa staa wa Bongo Movie, Kajala Masanja ameanika sababu ya kuanika mapema sura ya mtoto aliyemzaa hivi karibuni na mkali wa muziki wa kizazi kipya nchini, Marioo.

Akizungumza na Mwanaspoti, Paula aluiyejifungua Mei 3 amesema, sababu ya kwanza anajiamini na baba wa mtoto huyo, pia  kutaka pongezi ziweze kumiminika kwa wakati muafaka.

"Kwanza namshukuru Mungu kwa kujifungua salama, nina furaha ya kuitwa Mama na nimeamua kuonyesha sura ya mtoto mapema sababu sioni haja  ya kuendelea kumficha wakati amezaliwa na najiamini na baba wa mtoto, Omari 'Marioo'," amesema Paula na kuongeza;

"Sababu nyingine ni nikupata pongezi mapema, nataka zimiminike sasa, sio umejifungua leo pongezi zinakuja baada ya mwezi au miezi."

Kisura huyo, pia amefafanua kwa kusema yeye na mzazi mwenzie (Marioo) wameweka mazingira mazuri mtoto huyo aitwaye Amara, kiasi kitakachomfanya akue katika malezi bora.

"Tumekaa na kujadiliana na Baba Amara (Marioo) ili tutahakikishe dogo anakuwa katika mazingira mazuri, ikiwamo kumsomesha kadri ya uwezo utakavyoturuhusu," amesema Paula

Kitendo cha Paula  kuanika sura mapema ya mtoto mapema kimekuwa tofauti na baadhi ya wasanii wengi hapa Bongo waliofanikiwa kupata watoto kwani huwa wanazificha sura hadi siku ya 40 na wengine wametumia miezi kadhaa kuja kuziandika.

Miongoni mwa wasanii waliofanya hivyo, ni Diamond Platnumz na Zari, Aunty Ezekiel na Iyobo, Kusah, Nandy na BillNass, Jacklyne Wolper na Rich Mitindo, Elizabeth Michael 'Lulu' na Majizo na wengine.