Paten aumiza kichwa ujio wa wimbo mpya

Muktasari:
- Ukiwa na wiki mbili tangu kuachiwa kwakwe katika majukwaa ya kuuza na kusikiliza muziki, wimbo huo unaendelea kupata mafanikio makubwa huku ukikubalika zaidi ndani na nje ya nchi.
MSANII anayetamba na kibao cha Afande, Dogo Paten amesema licha ya kwa sasa kuwa bize na kufanya shoo, pia anaumiza kichwa kutoa nyimbo nyingine zitakazopendwa kama ilivyo kwa wimbo huo.
Dogo Paten alipata maarufu wiki chache zilizopita baada ya Zuchu kuupenda wimbo wa Afande na kumsapoti kwa kufanya remix.
Akizungumza na Mwanaspoti, Paten alisema "Mimi ni msanii na siwezi kubweteka kwa sasa, siwezi kuharakisha kutoa ngoma lakini nakaa chini kuumiza niweze kuwalisha vitu vizuri mashabiki zangu," alisema Paten.
Ukiwa na wiki mbili tangu kuachiwa kwakwe katika majukwaa ya kuuza na kusikiliza muziki, wimbo huo unaendelea kupata mafanikio makubwa huku ukikubalika zaidi ndani na nje ya nchi.
Msanii huyo hivi karibuni amechaguliwa kuwania tuzo za ‘EAEA Awards’ kama Best Singeli Fusion kupitia wimbo huo.
"Sina mengi ya kusema kwa sababu hayo yote ni mipango ya Mungu, lakini nashukuru sana kwa kuchaguliwa na hilo linanifanya niendelee kupiga kazi kuhakikisha malengo yangu yanatimia."