Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

P Diddy akutwa na hatia, ahukumiwa miezi 50 jela

Muktasari:

Diddy amehukumiwa miezi hiyo ambayo ni sawa na miaka minne na miezi miwili baada ya kukutwa na hatia ya makosa mawili yanayohusiana na usafirishaji wa watu kwa ajili ya biashara ukahaba.

Mwanamuziki wa Hip-hop na mfanyabiashara maarufu kutoka Marekani Sean “Diddy” Combs, amehukumiwa kifungo cha miezi 50 jela.

Diddy amehukumiwa miezi hiyo ambayo ni sawa na miaka minne na miezi miwili baada ya kukutwa na hatia ya makosa mawili yanayohusiana na usafirishaji wa watu kwa ajili ya biashara ukahaba.

Katika makosa hayo yaliyomponza Diddy, limo la kuwasafirisha wapenzi wake wawili wa zamani  Cassie na Jane na  kuwalazimisha kushiriki ngono na wanaume waliolipwa kwenye sherehe zilizoitwa 'Freak Offs'.

Diddy alikamatwa Septemba 16, 2024 katika hoteli ya Park Hyatt, Manhattan, New York na kupelekwa moja kwa moja katika gereza la Metropolitan.

Kesi yake ilianza kusikilizwa Mei 5,2025 huku watu mbalimbali wakitoa ushahidi akiwemo mpenzi wake wa muda mrefu Cassie Ventura, Jane, Mia, Kid Cudi, Bongolani, mama mzazi wa Cassie na wengineo.

Utakumbuka Serikali ilitaka Combs ahukumiwe kifungo cha kati ya miezi 51 hadi 63 jela, lakini kwa upande wa utetezi ulipendekeza kifungo kifupi cha kati ya miezi 21 hadi 27.