Mwanamuziki Defao afariki dunia

Tuesday December 28 2021
Defao PIC
By Mwandishi Wetu

Mwanamuziki wa Rhumba, Le General Defao Matumona amefariki dunia jana jioni Jumatatu Desemba 27, 2021 jijini Doula nchini Cameroon.
Defao alizaliwa Disemba 3, 1958 Kinshasa nchini Congo ni mwanamuziki mwenye uwezo wa kutunga nyimbo na kuimba na kucheza muziki.  
Familia imethibitisha kifo cha mwanamuziki huyo aliyefariki nchini humo alipokwenda kwa ajili ya kutumbuiza kipindi cha sikukuu.

Advertisement