Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mtoto anavyomtesa Wema Sepetu

Muktasari:

  • Sio mara ya kwanza kwa staa huyu kuweka wazi namna ambavyo anaumia kukosa mtoto hadi kufikia hatua ya kumuomba Tunda aliyezaa na mpenzi wake Whozu kumpa mwanae na kumfanyia sherehe kubwa mtoto huyo siku yake ya kuzaliwa.

STAA wa kike hapa nchini Wema Sepetu ameweka wazi namna gani anayakacha matukio yanayohusisha watoto kutokana na yeye kutobarikiwa mtoto hadi sasa.

Wema Sepetu mara nyingi amekuwa akionyesha kuumizwa na jambo hilo huku akiamini ipo siku na yeye Mungu atambariki kama alivyowabariki wengine.

Katika ukurasa wake wa kijamii wa Instagram mrembo huyo asiyechuja amesema hiyo ni moja ya madhaifu yake katika matukio kama hayo ashindwe kuudhuria.

Kauli hiyo nzito imemtoka alipoposti picha ya mke wa Petman akiwa mjamzito na kuandika maneno hayo ambayo yamegusa mioyo ya wachangiaji wengi.

"Leo niseme ukweli kutoka kwenye moyo wangu huwa najikuta siwezi kabisa kushiriki kwenye shughuli zinazohusu misiba au watoto kwasababu ‘cause’ zinanifanya nijisikie vibaya sana najikutaga nakosa pose na moyo wangu unaumia mnoo, .. nadhani kila mtu ana weakness zake kwenye maisha na mimi ni hiyo,"

"Au kwenda kwenye sherehe ambayo mwanzo mwisho utakutana na watu wanaongelea watoto tu huku wewe unakosa la kuongea kwenye mada unabaki unashangaa shangaa, najioneaga nijikalie zangu tu nyumbani kwakweli,"amesema Wema.

Romain Mai akasema "Ipo siku na sisi tutapata watoto wetu na kunyonyesha tuendelee kumtumaini Mungu anayeishi,"amesema,

Wengi katika posti hiyo walimpa maneno ya kumtia moyo na kumwambia aendelee kulia na Mungu wake kwa kuwa sio yeye pekee ambaye hajabarikiwa kupata mtoto.