Mke wa hulk ni balaa
Muktasari:
Na katika kuhakikisha hakuna mzozo wa kifamilia, aliamua kumpa Iran nusu ya mali zake ikiwa ni mijengo 40 kati ya 80 anazomiliki kule Brazil na kwingineko Ulaya.
MKWANJA unaweza kuhamisha mlima unaambiwa. Sasa talaka ya straika Mbrazil anayelipwa pesa ndefu kule China, Hulk inazidi kutawaliwa na drama kibao. Hulk ametangaza kutemana na mkewe Iran Angelo huku akimpa mgawo wa nyumba za kifahari kama 40 hivi na fedha kiasi cha dola za Marekani 100 milioni, lakini mwanamke huyo kagomea.
Baada ya kuishi pamoja kwa zaidi ya miaka 12 na kuzaa watoto watatu, Hulk aliamua kuivunja ndoa hiyo na kisha kuanzisha mahusiano mapya na mpwa wa Iran, Camila.
Na katika kuhakikisha hakuna mzozo wa kifamilia, aliamua kumpa Iran nusu ya mali zake ikiwa ni mijengo 40 kati ya 80 anazomiliki kule Brazil na kwingineko Ulaya.
Mbali na hilo, pia kampa hundi ya dola 100 milioni. Hata hivyo, ripoti zinasema kuwa, Iran kazigomea ofa hizo za Hulk na kusisitiza kuwa ni bora wakutane mahakamani kwani, Iran ana mpango wa kudai fidia kubwa zaidi ya ofa aliyopewa na mumewe huyo wa zamani.