Mkali wa wimbo wa 'Songi songi' kutua Bongo Oktoba 5

Wednesday September 29 2021
songi pic
By Nasra Abdallah

Mkali wa wimbo wa Songi Songi, Maud Elka, anatarajia kutua Bongo, Oktoba 5,2021.
 Hayo yameelezwa leo na msanii wa Bongo Fleva nchini Tanzania, Ally Saleh,maarufu kwa jina la Ali Kiba, alipokuwa akizungumzia ujio wa albamu yake mpya,anayotarajia kuiachia Oktoba 7 mwaka huu.
AliKiba na Maud walifanya remix ya wimbo wa Songi Songi na kuutoa Julai.Kabla ya hapo wimbo huo uliotoka miezi sita iliyopita ambapo msanii huyu kutoka  Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo alimshirikisha Hiro.
Katika mkutano wake huo  na waandshi wa habari leo, Alikiba alilolulizwa ni lini haswa ataachia video ya wimbo huo.
 Mwandishi alienda mbali na kueleza ni wimbo uliopekelewa vizuri lakini watu wanataka kujua lini haswa video yake itatoka kwani huenda ikafanya vizuri zaidi.
Katika majibu yake Ali Kiba amesema mashabiki watarajie video hivi karibuni na masanii huyo anatua nchini Oktoba 5,ambapo pamoja na shughuli nyingine watarekodi video.
“Ni kweli kumekuwa na uchelewaji wa kuachia wimbo,lakini ni kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo masuala ya janga la corona, lakini niwzhakikishie sasa mambo yanaenda vizuri na Muad atatua nchini Oktoba 5, kwa ajili ya shughuli hiyo ya kurekodi,”amesema Alikiba.
Ukiachilia mbali uzuri wa biti  la wimbo huo, umekuwa ukipendwa sana kutokana na namna ya uchezaji wake ambapo wapenzi walikuwa wakishindana kuucheza.
Katika wimbo huo,mbali ya Ali  Kiba kuimba kwa lugha ya kifaransa pia kaingiza Kiswahili.

Advertisement