Miss Tanzania 2022 kuondoka na Benz ya Sh40 milioni

Fainali za kumsaka mrembo atakayeiwakilisha nchi katika mashindano ya Miss World kufanyika kesho, huku mshindi atakayepatikana atazawadiwa gari aina ya Mercedes Benz C Class yenye thamani ya Sh40 milioni .
Sambamba na gari, pia mshindi huyo atapewa fedha Sh10 milioni.
Hayo yamesema na Meneja Masoko wa Star Media David Malisa, wakati wa mkutano na waandishi wa habari kuhusiana na fainali hizo ambazo zinatarajiwa kufanyika ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza katika hafla hiyo, Malisa amesema katika kinyang’anyiro hicho warembo 20 watapanda jukwaani kupambana na  mshindi kujizolea zawadi hizo.
Aidha Meneja huyo, alisema ukiachilia mshindi wa kwanza mshindi wa pili naye atajinyakulia Sh5 milioni, huku wa tatu atapewa Sh3 milioni na wan ne na wa tano watapewa kifuta jasho cha Sh1 milioni.
 “Tulisema tutatoa zawadi yenye thamani kubwa, ni hii ndio zawadi yenyewe ambayo tunaamini itamuheshimisha mrembo kama ambavyo shindano lenyewe linavyojielea kuwa urembo ni heshioma,”amesema Malisa.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Miss Tanzania Azama Mashangoambali na mshindi wa kwanza hadi wa tano, katika shindano hilo  pia kutakuwa na washindi wa vipengele tofauti walivyoshindanishwa wakati wakiwa kambini kwa takribani wiki mbili.
“Kwa namna tulivyowaanda warembo wetu kwa kipindi chote cha wiki mbili, tuna Imani wako tayari kuchuana ili kupatikana mshindi mmoja atakayekwenda kupeperuisha bendera ya nchi katika mashindano ya dunia hapo baadaye.

Mkurugenzi wa operesheni wa Kampuni ya Str8 Vibes, Damian Mapalala  alisema usiku huo utasindikizwa na burudani mbalimbali kutoka kwa wasanii mbalimbali akiwemo Bernad Paul “Ben Paul’ na Barnaba Elias ‘Barnaba Classic ‘.