Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mchekeshaji Molingo afariki dunia kwao Chato

Muktasari:

  • Taarifa ya kifo chake imetolewa na Mudi Msomali, aliyekuwa akiishi naye na kumsimamia katika sanaa yake.

Mchekeshaji Frank Patrick, maarufu  Molingo amefariki dunia usiku wa kuamkia leo Desemba 10,2024 nyumbani kwao Chato, mkoani Geita ambako alikuwa akiuguzwa na mama yake mzazi.

Taarifa ya kifo chake imetolewa na Mudi Msomali, aliyekuwa akiishi naye na kumsimamia katika sanaa yake.

"Inalilahi wainalilahi rajiun nimepambana imeshindikana. Pumzika kwa amani Molingo kwa yeyote atakayeguswa na msiba usiache kuwasupport kwao kwa chochote kesho tumsitiri Molingo,"ameandika Mudi kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Hata hivyo taarifa rasmi ya kilichosababisha kifo chake bado hazijatolewa. Utakukumbuka enzi za uhai wake Molingo (17) alikuwa akionekana kwenye video mbalimbali akichekesha na mwenziye Mudo, huku vichekesho vyao vingi vikiwa vya kubishana.
Mwananchi ilipomtafuta Msomali kuzungumzia hilo alijibu, “kweli amefariki ila naomba nitafute baadaye kidogo.”