Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mahrez, Sane watuliza mademu wao kishkaji

Muktasari:

Rita na Wilder ni marafiki wa karibu, jambo lililomfanya mchumba wake Wilder, Telli Swift kuingiwa hofu ya kuporwa. Swift anahisi kuwa Rita anaweza kuimpora bondia huyo kama ukaribu huo utazidi.

MASTAA wa Man City, Riyad Mahrez na Leroy Sane wameamua kumaliza ugomvi kati ya mademu wao kishikaji.

Mademu wa nyota hao waliripotiwa kuingia katika bifu na chanzo kikiwa, bondia Deontay Wilder. Kulingana na gazeti moja maarufu la udaku wa, mchumba wa Sane, Candice Brook ndiye aliyeanzisha zogo kwa kumnanga mke wake Mahrez Rita.

Candice alimtumia meseji za matusi kwa Rita, akimuonya kuacha tabia ya kujigonga kwa Wilder kwa kisingizio cha kujenga urafiki walionao.

Rita na Wilder ni marafiki wa karibu, jambo lililomfanya mchumba wake Wilder, Telli Swift kuingiwa hofu ya kuporwa. Swift anahisi kuwa Rita anaweza kuimpora bondia huyo kama ukaribu huo utazidi.

Candice ni rafiki mkubwa wake Telli na ndipo akacharuka na kuachia meseji za matusi.

Candice alimtusi Rita kwa kumtaka atulie na mchumba wake na akome kumfuata wa shogake.

Ugomvi huo ukaishia kuwahusisha wapenzi wao Sane na Maharez ambao wote wanaichezea City.

Lakini, kwa kuhakikisha zogo hilo halivurugi urafiki wao, wachezaji hao wamechapiana na kuamua kumaliza bifu hilo la mademu wao kishikaji na kimya kimya kwa kila mmoja kuhakikisha anamnyoosha demu wake bila kuleta vuzurugu.