Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Lulu: Nimepitia mambo mazito

Msanii wa filamu Elizabeth Michael maarufu kama Lulu akiweka shada la maua kwenye kaburi la aliyekuwa msanii mwenzake Steven Kanumba wakati wa kumbukumbu ya mwaka mmoja tangu kifo chake.

Muktasari:

  • Msanii huyo anakiri alitamani kuhudhuria mazishi ya mpenzi wake huyo, lakini haikuwa rahisi kwani alikuwa rumande.

MWIGIZAJI wa filamu Bongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’, amezungumzia historia ya maisha yake na matukio aliyopitia katika umri wake ambao katika hali ya kawaida ni mdogo kwa mhusika kuwa gumzo kwenye jamii.

Lulu alijikuta akiwa mahabusu ya Segerea baada ya mpenzi wake Steven Kanumba kufariki akiwa naye. Wengi walishangaa na kutoamini kuwa wasanii hao walikuwa  wapenzi kwani jambo hilo halikuwahi kujulikana.

Uhusiano na Kanumba

Lulu anasema yeye na marehemu walikuwa na uhusiano wa kimapenzi kwa muda mrefu, lakini moja ya makubaliano yao ilikuwa ni kuishi katika maisha ya siri hiyo. Katika hilo hataki kuzungumzia undani wa siri iliyokuwapo baina yao.

“Mapenzi yangu na Kanumba ilikuwa ni makubaliano yetu kufanya iwe siri, nadhani haikuwa na maana kwetu, mapenzi yalikuwa ya muda mrefu, lakini sitaki kuzungumzia uhusiano wetu kutokana mambo mengi yamepita,” anasema.

Msanii huyo anakiri alitamani kuhudhuria mazishi ya mpenzi wake huyo, lakini haikuwa rahisi kwani alikuwa rumande.

Anasema maisha ya mahabusu yamemjenga na kumfanya kuwa mtu tofauti. Anasema sasa anaona kuwa anao wajibu wa kutumia muda wake kupitia filamu, kuwaelimisha vijana na watu wazima kuhusiana na maisha.

Katika hilo anasema anaandaa filamu mbili ikiwamo ya ‘Mapenzi Ya Mungu’.

Anasema ‘Mapenzi Ya Mungu’ ameigiza kwa kushirikiana na Mama mzazi wa marehemu Kanumba (Flora Mtegoa).

Anasema filamu hiyo inaeleza kuhusu maisha yake alipokuwa rumande, kikubwa hapo anasema maisha ya huko yamemfanya amjue Mungu zaidi.

Lulu anasema kuwa filamu yake ambayo ipo tayari inasubiri kuzinduliwa wakati wowote ni ya ‘Foolish Age’ inayoelezea maisha yake na majanga aliyopitia.

Anaamini kuwa wakati mtu anapokuwa katika umri mdogo,  anaweza kufanya mambo ya hatari ambayo si rahisi kabisa kuyabaini kwa muda huo na hata kama akionywa hawezi kuelewa.

“Filamu ya Foolish Age inazungumzia jambo ambalo nina uzoefu nalo. Unajua katika umri wa namna hiyo mhusika anakuwa mbishi, hasikii hata akiambiwa,” anasema.

“Kupitia filamu hiyo ninaweza kuwafundisha watu mambo muhimu, nitafurahia kama nitawaokoa hata watu kumi kupitia kile nilichopitia mimi.”

Uhusiano na Mama Kanumba

Maisha ya Mama Kanumba na Lulu yamekuwa ya maelewano hata kuweza kuwafanya Mama Kanumba na Mama Lulu kuwa pamoja kwa nyakati tofauti.

Lulu anasema kuwa sasa wanaishi kama familia moja kila mtu anaelewa kilichotokea, ndio maana katika kuonyesha hilo wameigiza filamu pamoja.

Unapozungumza na Lulu kwa sasa, utabaini mabadiliko makubwa kwake kwani anaonyesha jinsi anavyoweza kuwafundisha wengine kupitia katika maisha yake.

Anasema awali alipoingia rumande alikuwa na mawazo mengi, lakini baadaye aliukubali ukweli na kujikuta akinenepa.

Marafiki

Kwake anahisi hajawahi kuwa na marafiki kwani ni vigumu sana kumjua rafiki wa kweli. Anasema katika mazingira yake huwa anakutana na watu kwa ajili ya kazi.

“Ninashindwa kufahamu kama ni kweli nina marafiki au la,  hata wale walioshindwa kuungana nami katika shida siwezi kuwalaumu,” anasema.

Mipango yake

Ni kumiliki kampuni ya utengenezaji filamu na kutayarisha filamu zake. Kwake jambo kubwa ni kuwa msanii mahiri atakayeitangaza nchi yake ya Tanzania na kuvuma ulimwenguni kote.

“Ninataka kuwa mfano kwa nchi yangu, kama ilivyo kwa Genevieve Nnaji au Noah Ramsey wa Nigeria, wameitangaza sana nchi yao wale, nafikiri nami wakati wangu umefika,” anasema.

Lulu anasema kuwa pamoja na wasanii hao kuwa mbali, lakini wanajulikana kila kona kutokana na ubora wa kazi zao.