Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Lonny Bway alamba shavu Marekani

Muktasari:

  • Staa huyo wa ngoma ya 'Wewe Hapo' aliyomshirikisha Marioo na iliyofanya vizuri katika mitandao ya kijamii ikiwemo Youtube ikiwa imeingiza zaidi ya watazamaji Milioni 13, muda mchache kupitia mitandao ya kijamii ya lebo hiyo wenye makao makuu Marekani ulitangaza kwa kumkaribisha kama mmoja wa wasanii.

MSANII wa muziki wa kizazi kipya, Lony Bway amepata dili la kutambulishwa katuika lebo ya muziki ya Onerpm ya Marekani.

Staa huyo wa ngoma ya 'Wewe Hapo' aliyomshirikisha Marioo na iliyofanya vizuri katika mitandao ya kijamii ikiwemo Youtube ikiwa imeingiza zaidi ya watazamaji Milioni 13, muda mchache kupitia mitandao ya kijamii ya lebo hiyo wenye makao makuu Marekani ulitangaza kwa kumkaribisha kama mmoja wa wasanii.

"Tukimpokea msanii wa Tanzania Lonybway kwenye familia ya ONErpm, hapa kuna kwa muziki mzuri tu," ulisomeka ujumbe huo ambao uliambatana na video ya msanii huyo.

Lebo hiyo inafanya kazi na wasanii mbalimbali akiwemo Chike wa Nigeria na kwa Tanzania wapo kina Ibrah wa Konde Gang, Obby Alpha na Zabron Singer.

Kwa sasa ONErpm inafanya kazi na nchi mbalimbali za Afrika ikiwemo Tanzania, Nigeria, Afrika Kusini, Ghana, Kenya, Ivory Coast lengo ni kuendeleza vipaji vya wasanii chipukizi wa muziki barani humo.