Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Lindsay Lohan : Haogopi kuchuma fedha kwa njia chafu

Muktasari:

  • Mwanamke huyo ana utajiri wa Dola 11 milioni.  Lindsay Lohan alianza umaarufu mwaka 2004 katika filamu ya vichekesho ya ‘Mean Girls’ ambayo iliuza nakala nyingi na kumfanya mwigizaji huyo kupata tuzo kibao licha ya umri wake mdogo.

Si vizuri kufuatilia maisha ya mtu, lakini kuna wakati  inaweza kutokea ukapenda kuyachunguza maisha ya mtu fulani kutokana na vituko vya mhusika.

Mwigizaji, Lindsay Lohan, ni miongoni mwa mastaa ambao huvuta hisia za wengi kwa sababu ya vituko vyake.

Mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 27 ambaye ni raia wa Marekani, anatikisa kwenye fani ya uigizaji ambayo imekuwa ikimpatia noti za uhakika.

Lakini kinachofanya amulikwe zaidi na vyombo vya habari au watu wa kawaida, ni namna ‘anavyojilipua’ katika matumizi ya fedha na vituko vya maisha kwa jumla. 

Mwaka jana Jarida la Forbes lilimtangaza mwanamke huyo kushika namba 30 kwa kusaka noti miongoni mwa waigizaji nchini humo.

Mwanamke huyo ana utajiri wa Dola 11 milioni.  Lindsay Lohan alianza umaarufu mwaka 2004 katika filamu ya vichekesho ya ‘Mean Girls’ ambayo iliuza nakala nyingi na kumfanya mwigizaji huyo kupata tuzo kibao licha ya umri wake mdogo.

Filamu za Lindsay na mauzo yake ni kama ifuatavyo; ‘Freaky Friday’ (Dola 550,000), ‘Confessions Of A Teenage Drama Queen’ (Dola 1 milioni), ‘Mean Girls’ (Dola 1,000,000) ‘Just My Luck’ (Dola7.5 milioni), ‘Georgia Rule’ (dola7.5 milioni),  ‘Liz And Dick’ (Dola 300,000) na ‘Scary Movie 5’ (Dola 200,000).

Lindsay hakuishia kwenye uigizaji, alijiingiza pia kwenye muziki ambao alikuwa akiutumia katika filamu zake.

Mwaka 2004 alitoa albamu ya muziki ya Lohan ‘Speak’ ambayo ilitikisa kwenye chati za Billboard.

Hakuishia kwenye muziki na filamu pekee, alipenya mpaka kwenye uanamitindo. Vile vile aliingia ubia kwenye kampuni za manukato.

Licha ya kusaka noti, dada huyo anafahamika kwa matumizi makubwa ya fedha ambayo yalimfanya akaribie kufilisika Oktoba 2011.

Baada ya kuona kipato chake kimeyumba, mwanamke huyo alipiga picha za utupu kwenye jarida moja Marekani na kupata Dola 1 milioni, fedha ambazo zilimwinua upya.

Matumizi mabaya

Pamoja na kipato hicho, Lindsay, hutumia fedha vibaya. Hupenda kununua nguo, viatu na vitu vingine ambavyo haviwezi kumsaidia kwenye maisha yake.

Mwaka 2009 alikodi nyumba na alikuwa akilipa Dola 10,000 kwa mwezi. Hutumia Dola 800 kwa wiki kwa ajili ya nywele. Mwaka 2011 alinunua gari aina ya Porsche kwa Dola 80,000.  

Skendo

Pamoja na kusaka noti, maisha ya dada huyo yameandamwa na skendo. Julai 2007 alifungwa jela kwa siku 90 baada ya kupatikana na hatia ya kufanya fujo, kukutwa na dawa za kulevya na kuendesha gari akiwa amelewa.

Katika miaka ya karibuni Lindsay amekuwa akienda kwenye mafunzo maalumu ya kuacha kutumia dawa za kulevya.