Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kajala avunja ukinya sakata la ugomvi na Harmonize

Muktasari:

  • Katika siku za karibuni, kwenye kurasa mitandao ya kijamii zimekuwa zikiripoti taarifa zikidai kuwa wawili hao hawapo sawa kimapenzi, jambo lililowafanya mashabiki wao kuanza kuhoji hatma ya penzi ambalo kwa muda mrefu limekuwa likifuatiliwa kwa karibu kutokana na historia yake yenye misukosuko.

Tetesi za kuwepo kwa mgogoro wa kimapenzi kati ya mwigizaji maarufu wa Bongo Movies, Kajala Masanja na msanii wa Bongo Fleva, Harmonize, zimeendelea kutawala mijadala kwenye mitandao ya kijamii huku baadhi ya mashabiki wakihusisha ukimya wao wa hivi karibuni na madai ya kuvunjika kwa uhusiano wao.

Katika siku za karibuni, kwenye kurasa mitandao ya kijamii zimekuwa zikiripoti taarifa zikidai kuwa wawili hao hawapo sawa kimapenzi, jambo lililowafanya mashabiki wao kuanza kuhoji hatma ya penzi ambalo kwa muda mrefu limekuwa likifuatiliwa kwa karibu kutokana na historia yake yenye misukosuko.

Hata hivyo, Kajala ameonekana kutokuwa na wasiwasi na maneno yanayoendelea kusambazwa mitandaoni, akisema hana cha kuzungumzia kuhusu tetesi hizo na kuwaachia wanaopenda kujadili maisha ya wengine kuendelea kufanya hivyo.

Akizungumza na Mwanaspoti kuhusu taarifa zinazoendelea kusambaa, Kajala amesema kwa kifupi; “Anawaachia wazungumzaji wa familia za watu watu wa mitandao.”

Kajala na Harmonize ni miongoni mwa mastaa ambao maisha yao ya kimapenzi yamekuwa yakivuta hisia za mashabiki kwa miaka kadhaa. Wawili hao waliweka wazi uhusiano wao mwaka 2021 kabla ya kupitia changamoto mbalimbali zilizosababisha kuachana na baadaye kurejeana tena.

Katika safari yao ya mapenzi, wawili hao wamewahi kuingia kwenye migogoro iliyozua mjadala mkubwa mitandaoni, lakini mara kadhaa walifanikiwa kurejesha uhusiano wao na kuendelea pamoja. Hali hiyo iliwafanya mashabiki wengi kuamini kuwa walikuwa wamejifunza kutokana na changamoto walizopitia hapo awali.

Mwishoni mwa mwaka jana, wawili hao walionekana kuwa karibu zaidi baada ya Harmonize kuweka wazi nia yake ya kufunga ndoa na Kajala, jambo lililoibua matumaini mapya kwa mashabiki wao. Hata hivyo, hadi sasa hakuna upande wowote uliothibitisha rasmi taarifa za kuachana zinazozungumzwa mitandaoni, huku kauli ya Kajala ikionyesha kuwa hataki kujihusisha na mjadala huo na ameacha watu waendelee kusema wanachotaka.