Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Julio na wenzake wamlilia Ruge

Muktasari:

 

Ruge Mutahaba alizaliwa mwaka 1970 katika mji wa Brooklyn, New York, Marekani. Alisoma Shule ya Msingi Arusha na Mlimani kabla ya kwenda Sekondari ya Forodhani na Pugu nchini Tanzania na baadaye alirudi tena Marekani kwa masomo ya Chuo Kikuu akisomea fedha.

Dar es Salaam. Wadau wa soka wamemlilia kwa uchungu aliyekuwa mmiliki wa Radio Clouds, Ruge Mutahaba aliyefariki dunia jana Jumanne nchini Afrika Kusini alipokuwa anatibiwa.

Kocha wa Dodoma FC, Jamhuri Kihwelo 'Julio' amesema, kwake ni kiongozi bora na amebadilisha maisha ya vijana wengi na wanaomzungumza vibaya waache.

"Duniani huwezi kupendwa na kila mtu hata mimi Julio wapo wanaonichukia na kunizungumzia vibaya lakini kwangu mimi Ruge ni mfano wa kuigwa. Vijana wengi wamepata mafanikio kwa sababu yake wakamiliki nyumba, magari na kusafiri nje ya nchi,"alisema Julio mchezaji na kocha wa zamani wa Simba.

"Amefariki, kikubwa ni kumwombea apumzike kwa amani kwa sababu sisi sote hapa duniani tunapita tu na huna sababu ya kumchukia mtu."

Meneja wa Azam FC, Philip Alando amesema, Ruge alikuwa zaidi ya mtu muhimu kwa taifa kutokana na namna alivyowainua sehemu kubwa ya wasanii.

"Kwetu kwenye mpira hakuwepo lakini upande wa sanaa na muziki wamefaidiaka kwa kiasi kikubwa kutokana na kuwakutanisha wadau hao. Ni maarufu kwa sababu ya vitu alivyokuwa anafanya kwa upande wangu nimesikitika."

Kocha wa Panoni FC inayoshiriki Ligi Daraja la Pili, Habibu Kondo amesema, Ruge ni mpambanaji na si kwamba anajipigania yeye mwenyewe tu bali watu wengine katika kujikomboa kimaisha.

"Tanzania imepata pigo hasa vijana kutokana na namna alivyokuwa mstari wa mbele kuwapigania kwa kuandaa makongamano mbalimbali namna ya kufanikiwa lakini pia waipende nchini yao,"alisema Kondo.

Amesema, amenyanyua wanamuziki wengi kimaisha na hajawahi kuona mtu kama yeye.