Huyu hapa msanii pekee ambaye Joe Biden 'amemfollow' Twitter

Rais mpya wa Marekani, Joe Biden aliapishwa jana Januari 20 huku tukio la kuapishwa kwake likisindikizwa na utumbuizaji kutoka kwa wasanii wakubwa wa muziki nchini Marekani wakiwemo Jennifer Lopez, Lady Gaga na Garth Brooks.

Na wakati hilo linaendelea, akaunti binafsi ya mtandao wa twiiter ya rais huyo ilikuwa ina-‘follow’ (wafuasi) akaunti zingine 46 tu na zaidi ni kwamba watu wote anaowa-follow Biden ni viongozi wa taifa hilo isipokuwa kwa akaunti moja tu ambayo ni ya msanii Lady Gaga.

Biden alianza kumfollow Lady Gaga tangu mwaka 2015 na mara kadhaa wawili hao wamekuwa wakitajana kwenye jumbe wanazoandika kupitia mtandao huo wa kijamii unaotumika zaidi na viongozi wakubwa wa serikali ya Marekani.

Awali Lady Gaga ambaye ametamba na vibao kama vile Alejandro alioekana kutoendana na raisi huyo kwani alikuwa akijiwasilisha kama msanii asiye na staha kama vile kuvaa nusu uchi hasa kwenye video za nyimbo zake, lakini kufafana kwa harakati zao za kupinga ukatili wa kijinsia kuliwaunganisha mwaka 2015.

Uswahiba ulianza baada ya mwaka 2014 Joe Biden kuanzisha kampeni iliyopewa jina la ‘Its On Us’ kwa ajili ya kupambana na kumaliza ukatili wa kijinsia. Ambapo mwaka 2014 huo huo Lady Gaga alijitangaza kuwa aliwahi kufanyiwa ukatili wa kijinsia zamani. Na mwaka 2015 alitangaza kuunga mkono kampeni iliyokuwa inaendeshwa na Joe Biden.

Kwa upande mwingine, akaunti rasmi ya rasmi ya mtandao wa Twitter ya raisi wa marekani ambaye kwa sasa ni Biden, inafollow jumla ya watu 12 huku 11 ikiwa ni viongozi wa taifa hilo, lakini moja ikiwa ni akaunti ya mwanamitindo Chrissy Teigen.

Akaunti hiyo inayofahamika kwa jina la @potus ambayo ni kifupi cha President Of The United States ilifollow akaunti ya Teigen jana baada ya kuapishwa; hata hivyo bado sababu haijabainika wazi.

Mbali na Biden, mwanamitindo Teigen amepigwa kufuli (block) kwa zaidi ya miaka minne kwenye mtandao huo na rais aliyepita wa nchi hiyo Donald Trump.

Kwenye mitandao mingine kama vile Instagram na Facebook Rais Biden amefollow wasanii wengi tu. Kwa mfano, akaunti yake ya Instagram ina follow watu 103, kati yao kuna zaidi ya wasanii 10 akiwemo muigizaji Dwayne Johnson ‘The Rock’, mchekeshaji Micheal Keegan, na waimbaji Jennifer Lopes, Luis Fonsi, Bill Elish na wengine.