Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

P Funky amzungumzia Kajala, Marioo apewa neno

Muktasari:

  • P Funk na Kajala ambao ni wazazi wa Paula aliyefanya sherehe ya mtoto wake wa kwanza aliyezaa na Marioo, walikuwapo katika pati hiyo pamoja na wageni wengine waalikwa huku pia Harmonize akionekana kuwa karibu na Kajala.

LICHA ya kuwepo kwa taarifa za Harmonize kurudiana na aliyekuwa mpenzi wake, Kajala Masanja, lakini hilo halijavunja uhusiano wa Produza maarufu wa muziki wa Bongo Fleva, Paul Matthysse 'P Funk-Majani' na amekiri mzazi mwenzake huyo bado ana upendo.

P Funk na Kajala ambao ni wazazi wa Paula aliyefanya sherehe ya mtoto wake wa kwanza aliyezaa na Marioo, walikuwapo katika pati hiyo pamoja na wageni wengine waalikwa huku pia Harmonize akionekana kuwa karibu na Kajala.

Mwanaspoti lililokuwepo katika sherehe hiyo ya kuzaliwa ya Amarah aliyefikisha mwaka mmoja na lilipata nafasi ya kupiga stori na mkali huyo wa biti mbalimbali zilizowatoa wasanii wengi na kufunguka na Dakika 5 Na... kuhusu pati hiyo na uhusiano wake na Kajala.


Baada ya kuelewana na Kajala unamzungumzia vipi kwa sasa?

"Kajala ni mzazi mwenzangu na siwezi mzungumzia vibaya kwa sasa, kwani amebadilika sana. Amekuwa msikivu na mwelewa sana hata katika mazungumzo, napenda na nampenda anavyotoa sapoti kwa Paula kuhusu malezi ya mjukuu wetu."


Kuhusu sherehe hii ya mjukuu wako Amara una lipi la kusema?

"Kwanza nimshukuru Mungu kwa kupata mjukuu na leo hii ametimiza mwaka mmoja na nimependa hii sherehe ilivyoandaliwa kwa asilimia kubwa imehudhuriwa na watoto, kiufupi imeleta lengo ya sherehe ya mtoto."


Unataka mjukuu wako awe wa namna gani?

"Natamani sana mjukuu wangu akikua na kujitambua awe mcha Mungu na asiwe mtu wa mitandao, unajua maisha mazuri kuyapata siyo tu mitandaoni, sababu hii mitandao kuna wapo watu wanaofeki maisha na wengine wako Real na wapo waliofanikiwa kimaisha bila ya kujionyesha mitandaoni. Hivyo, nina imani sana wazazi wake watamlea vyema tu."


Unadhani Amara ataweza kutokuwa mitandaoni ikiwa baba na mama ni staa?

"Kwa nini isiwezekane? Hivi ukichunguza hapa Bongo kuna wazazi mastaa wangapi na wamezaa watoto ambao jamii haiwafahamu na mambo yao yanaenda poa? Sasa kwa nini isiwe kwa Amara? Hapa inategemea na malezi ya wazazi na ndiyo maana nimekwambia natamani akikua asiwe mtu wa mitandaoni."


Toa neno kwa Marioo na Paula

"Neno langu ni moja tu, kuwataka waishi kwa upendo na Marioo awe baba bora na sio bora baba, wadumu pia kwenye mahusiano yao hadi waweze kufunga ndoa, hili ndilo jambo bora zaidi."


Sijamuona Mkongwe mwenzako Masta Jay hapa, mna bifu?

"Hapana hapana, sijawahi kuwa na bifu na Masta Jay, ila watu ndio walitaka tuwe na bifu na hii ilitengenezwa na mashabiki hasa wale tuliokuwa tunawafanyia kazi zao."