Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Huenda Ne-YO yakamkuta ya Diddy 

Muktasari:

  • Ne-Yo ameshambuliwa na mama huyo kwa maneno akimtuhumu kwa ukatili na kushiriki ngono mbele ya watoto wake, kujihusisha na madawa ya kulevya na unyanyasaji dhidi yake

Mama watoto wa mwanamuziki kutoka nchini Marekani, Ne-Yo anayefahamika kwa jina la Big Sade, amemfananisha msanii huyo na Diddy kwa kumuita 'Diddy Junior'.

Kwa mujibu wa Tmz News limeeleza kuwa mwanamke huyo amedai kuwa Ne-Yo ni mmoja kati ya watu wanaoelekea kuumbuka kama Diddy kwa tabia zake chafu.

Ne-Yo ameshambuliwa na mama huyo kwa maneno akimtuhumu kwa ukatili na kushiriki ngono mbele ya watoto wake, kujihusisha na madawa ya kulevya na unyanyasaji dhidi yake.

Hivi karibuni Sade alirekodi video ya majibizano yake na msanii huyo na kuirusha mitandaoni ambapo alitoa shutuma hizo na huenda Ne-Yo ni mmoja kati ya wanamuziki wanaofuata kuumbuliwa nchini humo.

Msanii huyo amewahi kufanya nyimbo kama Give me Everything, Closer, Mad, So Sick, Because of You, Miss Independent, She Knows, Time of Our Lives. Pia miaka 7 iliyopita aliwahi kufanya kolabo na DiamondPlatnumz katika wimbo wa ‘Marry You’.

Ikumbukwe kuwa Machi 2, makazi ya Diddy ya Los Angeles na Miami yalifanyiwa upekuzi na Mawakala wa Usalama wa Taifa kama sehemu ya uchunguzi wa serikali kuhusu madai ya biashara ya ngono yanayomhusisha msanii huyo.