Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Harmonize agonga kolabo ya kibabe na mastaa kibao Ghana

Hermonize Pict

Muktasari:

  • Katika kolabo hiyo, mbali na Harmonize, KJ amemshirikisha mwimbaji mwingine, mkali wa Dancehall kutoka Jamaica, Konshens ambao kwa pamoja wamenogesha singo hiyo.

MSANII wa Bongo Fleva, Rajab Abdul 'Harmonize' ameshirikishwa na staa wa muziki kutoka Ghana, KJ Spio katika kibao kiitwacho 'Messi".

Katika kolabo hiyo, mbali na Harmonize, KJ amemshirikisha mwimbaji mwingine, mkali wa Dancehall kutoka Jamaica, Konshens ambao kwa pamoja wamenogesha singo hiyo.

Ngoma hiyo  imetayarishwa na mshindi wa Tuzo ya Grammy, Mjamaika Izzy Beats, aliyefanya pia kazi za wakali kama Jorja Smith, Rema, Koffee, Masego, Alicia Keys na wengineo, ina mikito ya Afrobeats, Dancehall na Amapiano.

Mchanyato wa wasanii hao, KJ Spio, Harmonize na Konshens, unajifanya ngoma hiyo kuwa ya aina yake na isiyochosha masikioni mwa msikilizaji.

Akizungumzia wimbo huo, KJ Spio anasema: "Mimi ni shabiki mkubwa wa Konshens, na baada ya kufanya kazi na Harmonize awali, niligundua kwa pamoja tunaweza kufanya kitu kizuri. Kwa hiyo nikachukua uamuzi huo na kilichotokea kinakwenda kutengeneza historia."

Harmonize naye akizungumzia ushiriki wake katika singo hiyo alisema: “Huu wimbo ni mzuri sana kuwahi kutokea. Ni muziki wa kimataifa, utasumbua sana ndani na nje ya bara letu la Afrika."

Konshens akasema: "Kufanya kazi na Harmonize na KJ Spio ni ushiriki mzuri, tulipata muda mzuri wa kuandika, kukagua ala za muziki na hatimaye kurekodi video. Ninapenda sana muziki kutoka kwetu. Ni kazi nzuri sana kwa hakika."