Familia ya Mandojo yataja msiba ulipo

Muktasari:
- Akizungumza na Mwananchi mdogo wa marehemu, Yohana Chacha amesema kuwa mwili bado upo kwenye chumba cha kuhifadhia maiti lakini msiba upo kwake Mtaa wa Ndachi nyuma ya shule ya Sekondari ya Mnadani jijini Dodoma.
Msiba wa mwanamuziki na mfanyabiashara, Joseph Francis maarufu Mandojo kwa siku ya leo upo Dodoma kwa ajili ya taratibu nyingine za mazishi.
Akizungumza na Mwananchi mdogo wa marehemu, Yohana Chacha amesema kuwa mwili bado upo kwenye chumba cha kuhifadhia maiti lakini msiba upo kwake Mtaa wa Ndachi nyuma ya shule ya Sekondari ya Mnadani jijini Dodoma.
"Msiba upo nyumbani kwangu panaitwa Ndachi nyuma ya Shule ya Sekondari Mnadani barabara kuu iendayo Singida kwa afande Yohana Chacha, mwili bado upo chumba cha kuhifadhia maiti tunasubiri ndugu wengine wafike,"amesema.
Mandojo amefariki dunia leo Jumapili Agosti 11, 2023 wakati akipatiwa matibabu hospitalini mkoani Dodoma.
Enzi za uhai wake aliwahi kutamba na ngoma kama vile Nikupe Nini, Dingi, Muziki Chacha na nyingine nyingi akiwa na mwanamuziki mwenzake Domo Kaya.