Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Facebook yamponza Flora Mbasha

Flora Mbasha

MWANDISHI WETU MTANDAO maarufu wa kijamii wa Facebook umemponza msanii mahiri wa muziki wa injili nchini Tanzania, Flora Mbasha, baada ya mtu asiyefahamika ambaye ni shabiki wake kugandisha picha chafu ya ngono kwenye ukurasa wake ambayo iliibuka mijadala na kushangaza wengi wiki iliyopita. Mbasha aliyetamba na nyimbo kama 'Adui', 'Usife Moyo', 'Sauti ya Mnyonge' aliibuka kwenye mtandao huo na kutoa ufafanuzi kama ifuatavyo; "Bwana Yesu asifiwe wapendwa, naomba niwatake radhi kwa picha ambayo ilikuwa imetupiwa kwenye ukurasa wangu pia niwashukuru wote ambao mmenipigia simu kunieleza kinachoendelea kwenye Facebook yangu, pia nawashukuru wote mlionielekeza jinsi ya kuifuta maana nilijaribu nikashindwa. Lakini pia niombe anayetupia picha kama hizi kwenye ukurasa wangu aache upesi la sivyo nitaifunga mtu yeyote asitupie vitu vyake ingawa haikuwa nia yangu kuifunga kwani hii ni kwa ajili ya injili watumishi wa Mungu kukutana kuzungumzia habari za Mungu na marafiki mbalimbali kuelimishana kuhusu injili na mambo yote yenye maadili na siyo jambo lolote ambalo halimpendezi Mungu. Kwa upande wangu nimekwazika sana kwani sikutegemea kama mtu mwenye akili timamu angefanya hivyo, ila nimemsamehe, nia yangu ni nzuri sana nataka watu tujadili mambo ya Mungu, tushauriane na hasa kutokana na huduma ya uimbaji niliyo nayo nahitaji sana ushauri wenu na mawazo, pia niwashirikishe mambo mbalimbali kuhusu maisha yangu binafsi pamoja na huduma, ili kwa pamoja tuonyane na tusaidiane, pia tuombeane. Nawapenda sana wote na amani ya Yesu Kristo iwe nanyi.