Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Diva, Niffer kuhojiwa na polisi Dar

Michango Pict
Michango Pict

Muktasari:

  • Hayo yamebainishwa leo Jumanne Novemba 19, 2024 katika taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro.

Jeshi la Polisi linawashikilia kwa mahojiano ya kina Diva Malinzi (36) na Jenifer Jovin (25) maarufu Niffer kwa tuhuma za kuchangisha fedha kwa ajili ya walioporomokewa na ghorofa eneo la Kariakoo.

Hayo yamebainishwa leo Jumanne Novemba 19, 2024 katika taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro.

“Watuhumiwa wawili wamekamatwa na wanahojiwa kwa kina. Waliokamatwa ni Diva Gissele Malinzi miaka 36, mkazi wa Mikocheni amekamatwa Dar es Salaam na Jenifer Jovin miaka 25, mkazi wa Salasala Kinondoni ambaye amekamatwa Dodoma na kurejeshwa Dar as Salaam,” inaeleza taarifa hiyo.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Jeshi la Polisi litashirikiana na mamlaka zingine za kisheria kuona hatua zinazopaswa kuchukuliwa dhidi ya watuhumiwa hao.

Jengo hilo liliporomoka Jumamosi Novemba 16, 2024 na kusababisha vifo vya watu 16 na wengine zaidi ya 80 kujeruhiwa.