Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Diamond Platnumz: Nikioa mke wa pili kuna mtu anateseka?

Muktasari:

  • Tetesi hizo zimesambaa katika baadhi ya mitadao ya kijamii, huku baadhi ya watumiaji wa mitandao wakidai kuwa staa huyo ameamua kuongeza mke mwingine jambo lililozua mjadala mkubwa miongoni mwa mashabiki wake.

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz ameingia katikati ya mjadala wa mitandaoni baada ya kuibuka kwa madai yanayodai kuwa ameoa mke wa pili miezi michache baada ya kuthibitisha ndoa yake na msanii mwenzake, Zuchu.

Tetesi hizo zimesambaa katika baadhi ya mitadao ya kijamii, huku baadhi ya watumiaji wa mitandao wakidai kuwa staa huyo ameamua kuongeza mke mwingine jambo lililozua mjadala mkubwa miongoni mwa mashabiki wake.

Akizungumzia madai hayo, Diamond alionekana kushangazwa na namna watu wanavyofuatilia kwa karibu maisha yake binafsi na kuhoji kwa nini suala la ndoa yake linapaswa kuwa mjadala wa umma.

“Nikioa mke wa pili, kuna mtu anateseka? Kuna mtu nimemnyang’anya mke wake au nimemdhulumu mtu?” alihoji Diamond Platnumz.

Kauli hiyo imekuja mwaka mmoja baada ya kuweka wazi kwamba yeye na Zuchu wamefunga ndoa ya Kiislamu kwa siri. Awali taarifa za ndoa yao zilianza kuibuka mwezi Juni 2025 baada ya picha za hafla yao ya ndoa kusambaa mitandaoni kabla ya kuthibitishwa na pande husika.

Zuchu mwenyewe aliwahi kuthibitisha kuwa ni mke halali wa Diamond, huku Sheikh Walid Kawambwa akieleza kuwa ndiye aliyefungisha ndoa hiyo miezi kadhaa kabla ya kuwekwa wazi hadharani.

Kwa mujibu wa taarifa zilizowahi kuripotiwa na vyombo mbalimbali vya habari, ndoa hiyo ilifungwa kwa faragha huku Diamond alikiri kuwa waliamua kuiweka siri ili kutenganisha maisha yake binafsi na shughuli zake za muziki.

Diamond na Zuchu wamekuwa katika uhusiano wa muda mrefu uliogubikwa na vipindi vya kuachana na kurudiana, jambo ambalo limewafanya kuwa miongoni mwa wanandoa wanaofuatiliwa zaidi kwenye tasnia ya burudani Afrika Mashariki.

Safari yao ya mapenzi imekuwa ikizalisha mijadala mikubwa kila mara kunapotokea jambo jipya kuhusu maisha yao.

Licha ya madai ya kuoa mke wa pili kuendelea kusambaa, hadi sasa hakuna uthibitisho rasmi uliowekwa hadharani unaothibitisha kuwepo kwa ndoa nyingine ya Diamond. Hata hivyo, kauli yake imeonyesha wazi kuwa hana tatizo na mjadala huo, akisisitiza kuwa maamuzi yake ya ndoa hayapaswi kuwa chanzo cha maumivu kwa watu wengine.