Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Diamond alivyotumia 'Copy and Paste' ya Ibraah kumjibu Harmonize

MONDI Pict

Muktasari:

  • Harmonize ametafsiri kitendo hicho ni kama kejeli na kuamua kujibu kwa kutumia kwa kuweka 'screen shot' ya picha ya Diamondi aliyoposti wimbo huo.

Wakati sakata la Harmonize na Ibraah la kudaiana Sh1 bilioni likiendelea, mengine yameibuka baada ya Diamond kuingilia kati baada ya kuposti wimbo mpya wa Copy and Pest huku wengi wakidai sakata hilo ni kama lililomtokea yeye.

Ni hivi. Ibraah baada ya kutoa wimbo wake wa Copy and Pest siku tatu zilizopita, ulimfikia Mondi na kuamua kuuposti katika ukurasa wake wa Instagram akiambatanisha na picha yake, kitendo ambacho kilimkera Harmonize.

Harmonize ametafsiri kitendo hicho ni kama kejeli na kuamua kujibu kwa kutumia kwa kuweka 'screen shot' ya picha ya Diamondi aliyoposti wimbo huo.

Mmiliki huyo wa lebo ya Konde Gang, aliweka picha hiyo ikisindikizwa na maneno yanayodhaniwa ni kama Diamondi ameweka makusudi ili ionekane kama anamhitaji Ibraah kwenye lebo yake ya Wasafi. Harmo pia aliandika maneno ya kukashifu shoo ya Mondi aliyoifanya Tarime hivi karibuni.

Hata hivyo, mashabiki wamekuwa na mitazamo tofauti kutokana na chapisho hilo la Harmonize wakimjia juu kwamba Mondi kutumia wimbo wa Ibraah haimaanishi anataka kumchukua Ibraah, bali malipo ni hapa hapa duniani kutokana na kile kilichotokea baina yao wakati Konde Boy akiondoka lebo ya Wasafi. Ndiyo maana ya kucopy na kupest.

Shabiki wa kwanza aliongea na Mwanaspoti na kudai; "Mimi kwanza nimemshangaa sana Harmonize kwa kitendo alichokifanya cha kujibu vile baada ya kuona Diamondi katumia wimbo Ibraah copy na kupest. Kwa tulioelewa ni anamaanisha ni kama yale yaliyotokea kwake baada ya kutakiwa kulipa milioni 600 akawa anamlalamikia ni nyingi na alikuwa anaongea sana," anasema shabiki huyo.

Shabiki mwingine aliandika; "Diamond kutumia wimbo wa Ibraah kuposti picha yake mie naona hakuna tatizo kwani mwenyewe alishasema Ibraah na Anjella kabla hajatoka lebo ya Konde Gang ni wajukuu zake, sasa babu kuposti wimbo wa mjukuu kuna tatizo gani?" anahoji.

Hata hivyo, Mwanaspoti lilimtafuta Diamondi Platnumz ili awefafanue zaidi kuhusu jambo hilo lakini simu yake ya mkononi ilikuwa inaita bila kupokelewa.