Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Cholo Kobis: Jamii inanielewa vibaya

CHOLO Pict

Muktasari:

  • Cholo ambaye ameigiza kama kibaka au mtukutu kwenye tamthilia hiyo, amesema kwenye maisha yake ya uhalisia ni mtu wa ibada sana, lakini hakuna mtu anaweza kuelewa kutokana na kazi anayoifanya.

MSANII anayefanya vizuri katika tamthilia ya Kombolea, Farid Mohammed ‘Cholo Kobis’ amesema tamthilia hiyo imemtambulisha kwa jamii, lakini anachukiwa na baadhi ya wazazi wasiofahamu ni maigizo tu.

Cholo ambaye ameigiza kama kibaka au mtukutu kwenye tamthilia hiyo, amesema kwenye maisha yake ya uhalisia ni mtu wa ibada sana, lakini hakuna mtu anaweza kuelewa kutokana na kazi anayoifanya.

“Maisha yangu binafsi na Kombolela ni vitu viwili tofauti, lakini licha ya yote anayoyapitia hasa kwenye kuchukiwa anajivunia kwani anaamini anachokifanya kinaifikia jamii vizuri na wanakielewa,” amesema na kuongeza, siku ya kwanza wanamwambia anatakiwa kuigiza aina ya maisha hayo alikuwa tayari amepata picha ya kuna mashabiki watakaomkubali na watakaomchukia.

Akizungumzia tamthilia hiyo kwa jumla, amesema imempa jina kubwa na kazi zaidi, huku akiwataka waandaaji kumpigia simu kwani bado anataka mafanikio zaidi.”