Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Chanzo kifo cha mchekeshaji Molingo chatajwa

Muktasari:

  • Molingo amefariki dunia usiku wa kuamkia leo Desemba 10,2024 nyumbani kwao Chato, mkoani Geita ambako alikuwa akiuguzwa na mama yake mzazi.

Mudi Msomali aliyekuwa akimsimamia marehemu mchekeshaji Frank Patrick, maarufu Molingo katika sanaa yake, amesema kijana huyo aliishiwa damu baada ya kumtoka kwa saa tano.

Molingo amefariki dunia usiku wa kuamkia leo Desemba 10,2024 nyumbani kwao Chato, mkoani Geita ambako alikuwa akiuguzwa na mama yake mzazi.

"Alikuwa na tatizo la kuishiwa damu kwa muda wa miezi miwili. Mwezi wa tisa akawa ametoka kwenda kutafuta kazi, Oktoba 4,2024 akarudi akaniambia anaumwa Malaria nikampatia dawa, alikuwa amevimba uso akatumia dawa uso ukawa umerudi vizuri.”

"Siku mbili zikapita akaanza kutokwa na damu nyingi sana puani nikamuwahisha zahanati ya hapa jirani ikashindikana. Damu zikagoma kukata tukampeleka Hospitali ya Mkoa wakamshughulikia kuanzia saa sita damu zilikuja kukata saa 11 jioni," amesema Msomali.

Amesema baada ya hapo alipelekwa Hospitali ya Wilaya ya Geita kwa matibabu zaidi na kuruhusiwa kutoka hospitali Desemba 2,2024, akaenda nyumbani kwa baba yake mzazi, ambapo alikuwa akitokea nyumbani kwenda kuongezewa damu.

"Juzi akatoka kwa baba yake akaenda nyumbani kwa mama yake mzazi Chato, ambapo ndipo alikofariki. Tunategemea kumpumzisha leo Desemba 10,2024 katika kijiji cha Katoro,"amesema Mudi.